November 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TVLA,yapongezwa kwa kuzalisha chanjo

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, imeipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwa uzalishaji wa chanjo za mifugo ambazo zinatumika kuboresha afya za mifugo hapa nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo,Dedatus Mwanyika kwa niaba ya kamati hiyo,walipotembelea Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Kibaha, Mkoa wa Pwani Novemba 12, 2024.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Alexander Mnyeti,amesema mipango ya Wizara ni kuendelea kuhamasisha pamoja na kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu umuhimu wa kuchanja mifugo

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya VeterinariT anzania (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi, amesema kwa sasa wameanza kuwafikia wafugaji moja kwa moja kuwapa elimu ya umuhimu wa chanjo kwa mifugo yao.

Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) ipo chini ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ambapo jukumu lake kubwa ni kufanya tafiti na kuzalisha chanjo.