January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tutapata ushindi wa kishindo Kigoma

Na Penina Malundo, TimesMajira Online, Kigoma

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amesema kutokana na wasanii wa Mkoa wa kigoma kukiunga chama chao mkono ni dhahiri watashida kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, 2020.

Akiongea katika uwanja wa lake Tanganyika Mkoani
kigoma, Dkt. Magufuli amewapongeza wasanii ambao wengi wao wanatokea kigoma kwa kitendo cha kumuunga mkono jambo linalompa uhakika kuwa apatapa ushindi wa kishindo.

“Wasanii hawa ni wa hapa wengi wamezaliwa hapa, tunaamini tunaenda kushinda nataka kuibadilisha zaidi Kigoma hivyo tunaomba mtuchagueni sisi ili kuja kukamilisha kazi katika kipindi cha miaka mitano ijayo,” amesema Dkt. Magufuli.

“Lakini pia nawapongeza wasanii wote wanaojitokeza kunadi sera za Chama cha Mapinduzi, hivyo wananchi wa hapa msiache kuipigia kura CCM, Oktoba28,mwaka huu,”.

Wasanii waliopanda kunogesha jukwaa la mkutano wa Kampeni wa Chama hicho ni pamoja na kundi la Wanaume TMK kutoka Temeke, Linex Sunday, Ali Saleh Kiba na Rajab Kahali(Harmonize).