December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tunda aweka hadharani ujauzito wake

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

BAADA ya muda mrefu kukana kuwa hana ujauzito, hatimaye Video Vixen maarufu hapa nchini Cappuccino Tunda ameuweka hadharani Ujauzito wake na kusema muda si mrefu anatarajia kuitwa mama.

Tunda ambaye amejizolea umaarufu mwigi katika mitandao ya kijamii, anatarajia kupata mtoto huku mchumba wake msaii wa muziki wa Bongo fleva whozu akiwa mwenye furaha baada ya mpenzi wake huyo kuwa mjauzito.

“Karibu Duniani Mwanangu huku Mimi na Mama yako tunakusubiri kwa hamu sana. Na leo (jana) ndo siku ya Baby shower yako. Basi mwanangu Mimi baba yako wala sina maneno mengi we chagua ufanane na Mama yako au mimi utakavyopenda wala usijali. Ila itapendeza sana mwanangu ukifanana na Mama yako kwa sababu Mama ni Pisi kali

“Eeh Mungu sisi sote tunajikabidhi mikononi mwako ikawe heri na faraja kwetu.Utulinde na wenye roho mbaya, Roho za husda na wasiotupenda. Nakupenda sana Mama K,” amesema whozu.

%%%%%%%%%%%%%