January 7, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meneja mkuu Jajian Saimon akizungumziia namna taasisi ya wakala Sangeni International inavyofanyakazi na vyuo vikuu mbalimbali

Meneja Sangeni International awakumbusha wazazi kutumia mawakala kupata udhamini elimu nje ya nchi

Na Bakari Lulela,TimesMajira Online, Dar

WITO umetolewa kwa wazazi na walezi kutumia wakala wanaotambuilika kisheria ili kuepuka udanganyifu katika kuwatafutia vijana wao nafasi za kujiunga na masomo ya elimu ya juu nje ya nchi.

Wito huo umetolewa na Meneja wa Sangeni International, katika Maonesho 16 Elimu ya Juu ya Sayansi na Teknolojia Meneja mkuu Jajian Saimon amesema kwamba wazazi na walezi ni vizuri wakashirikiana katika kutafuta vyuo ili kuepukana usumbufu utakaowapata.

“Ninatoa rai kwa wazazi na walezi kutumia wakala wanaotambulika kisheria pindi wanapowatafutia vijana wao nafasi za masomo ya elimu ya juu kwenye vyuo mbalimbali nje ya nchi, ” amesema Saimon

Aidha Saimon amesema kwa kuzingatia ubora wa kuendeleza elimu taasisi hiyo imejikita kuwatafutia vijana vyuo vilivyo bora sambamba na kufuatilia kwa karibu mwenendo wa wanafunzi kipindi chote wawapo masomoni.

Sangeni imebobea katika kuwatafutia vyuo vyenye sifa ambavyo hutambulika pamoja na kuwatafutia kazi mara baada ya wanafunzi kuhitimu masomo yao.

Meneja huyo amewataka wazazi na walezi kutembelea banda la Sangen katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam kupata maelezo namna ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu vilivyoko nje ya nchi.

Maonesho hayo yameanza Julai 26 ambapo leo mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako anatarajia kuyafungua na yamebeba kauli mbiu “Kuendelea kukuza na kudumisha uchumi wa kati kupitia elimu ya juu, sayansi na teknolojia.”