November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tume ya umwagiliaji kuifanya sekta ya umwagiliaji kuwa endelevu

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

TUME ya Taifa Umwagiliaji ifanikiwa kukusanyankiasi cha shilingi bilioni mbili kwa mwaka 2024 kutokana na ada za wakulima wanaotumia skimu za umwagiliaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza na waansishi wa habari kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji (88) yanayoendelea jijini Dodoma Ofisa Kilimo Mwandamizi kutoka Tume hiyo Lukombeso Udumbe amesema ,fedha zinazopatikana katika makusanyo ya ada za wakulima zinatumika kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa skimu nyingine ili kufanya uendelevu wa sekta ya umwagiliaji .

Aidha amesema kiasi hicho kimeongezeka kutoka milioni 150 mwaka wa fedha 2021/2022 huku akisema hayo ni mafanikio makubwa.

Amesema mbali na tozo hiyo, nusu ya bajeti ya Wizara ya Kilimo kuanzia mwaka 2022/2023 na 2023/24  ilikwenda kwenye tume hiyo kwa ajili ya skimu za umwagiliaji

Aidha amesema ada hiyo ni tozo ambazo hutolewa na wakulima katika maeneo ya skimu za umwagiliaji huku akisema tozo hiyo ipo kwa mujibu wa sheria .

Kwa mujibu wa sheria ya Tume ya 2013, namba nne, imeipa Tume ya Umwagiliaji  jukumu la kuhakikisha wakulima wanatia tozo katika skimu ambazo uwekezaji umefanyika  wanapoanza kuzalisha.

Amesema kufatilia makusanyo hayo,Tume imeendelea kuongeza eneo la umwagiliaji ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Aidha amesema kazi iliyofanyika ni pamoja na kujenga mabwawa makubwa kwa lengo la kuvuna   maji yaliyokuwa yanapotea.