December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tulia Trust yawakosha mashabiki Mbeya City

Na Esther Macha, Timesmajira,Online, Mbeya

TAASISI ya Tulia Trust katika kuhakikisha timu ya Mbeya City inasonga mbele taasisi hiyo imezindua jezi za mashabiki wa timu hiyo kwa kata zote 36 Jijini Mbeya lengo likiwa ni kuhamasisha masuala ya michezo .

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jezi hiyo Ofisa Mawasiliano wa taasisi ya Tulia Trust , Joshua Edward amesema kuwa si mara ya kwanza kwa taasisi hiyo chini ya Mkurugenzi wake ambae ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson kugawa jezi za mashabiki.

Amesema kuwa ugawaji jezi hizo ni kwa awamu nyingine pamoja na kuunga mkono jitihada za mashabiki,wachezaji pamoja na viongozi wa timu ya Mbeya City ya Jiji la Mbeya.

“Si mara ya kwanza kwa taasisi yetu kugawa jezi hizi,hii ni awamu nyingine lengo likiwa ni kuhamasisha suala la.michezo jijini hapa kupitia Mbunge wetu na Mkurugenzi wa Tulia Trust,”.