Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inaendelea na mkakati wake wa kutangaza utalii wa Tanzania kupitia mashindano ya michezo ya kimataifa ambapo leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa Klabu ya
Magnet Youth Sport Organization ya jijini Dar es Salaam.
Klabu hii inatarajia kuiwakilisha nchi ya Tanzania katika mashindano ya kombe la Gothia yatakayofanyika nchini Sweeden
Kombe la Gothia ni mashindano ya kimataifa ya chama cha vijana cha mpira wa miguu kilichoandaliwa na kilabu cha kitaalam cha mpira wa miguu BK Häcken, ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka tangu 1975
katika mji wa Gothenburg, Sweden.
Mashindano ya kombe la Gothia yanahusisha vijana kati ya miaka 11 mpaka miaka 13 ambapo jumla ya timu 1,606 kutoka nchi 59 duniani zinategemea kushiriki katika mashindano haya.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika viwanja vya TPDC jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Felix John amesema kuwa michezo ni moja ya mazao ya utalii,
hawa ni vijana wadogo ambao tunawaangalia kwa jicho la kimkakati wa tutumia fursa wanazopata za kushiriki mashindano ya kimataifa kutangaza utalii wa Tanzania.
Aidha, TTB inapandikiza mbegu kwa vijana hawa ya kupenda michezo pamoja na utalii, kwani kupitia michezo itawasaidia kuwa wazalendo na hatimaye kuwa na shauku ya kutangaza vivutio vya nchi ya
Tanzania. Ametoa rai kwa Wanamichezo kuhakikisha wanafanya vizuri ili waweze kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia mashindano hayo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Klabu ya Magnet Youth Sport Organization, Tuntufye Mwambusi ameishukuru Bodi ya Utalii Tanzania kuwakabidhi Jezi hizo vitatumika kama nyezo za kutangaza utalii wa
Tanzania na kuhakikishia umma kwamba timu zote tatu zimejitayarisha vizuri na wana na matumaini ya kufanya vizuri.
Jumla ya wachezaji 46 wanaatajia kuondoka kesho, mwaka 2019 klabu ya Magnet iliweza kuiwakilisha Tanzania, Safari hii itakuwa mara ya pili kushiriki katika mashindano haya.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025