December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TTB: Biashara ya utalii yakua nchini

Na Mwandishi wetu,Timesmajira online

SERIKALI kupitia Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) imesema kuwa biashara utalii imeendelea kukua kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa kuleta matunda ndani ya taifa.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam Aprili 28 na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Damasi Mfugale wakati akifunga mafunzo ya siku moja kwa.waandishi wa habari za mtandaoni ambayo yalilenga kuwajengea uwezo wa namna ya kuandika habari zinazohusu Utalii yaliandaliwa na Chama Cha waandishi wa vyombo vya habari TAMPA
, Chuo Cha Taifa Cha Utalii na kufadhiliwa na Shirika la Hifadhi la Taifa.

Amesema biashara ya Utalii imekuwa kutokana na watu kuamasika kwenda kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo ndani ya nchi .

“Mafanikio haya ni matokeo ya jitihada mbalimbali ambazo nchi imekuwa ikifanya katika kuendeleza sekta ya Utalii”amesema

Amesema miongoni mwa jitihada hizo pamoja na kutagaza vivutio vya Utalii ndani na nje ya nchi ni pamoja na filamu ya Royal Tour.

” Filamu ya Royal Tour imeendela kuleta mafanikio makubwa katika sekta ya Utalii kabla ya mlipuko wa UVIKO 19 mapato yatokanayo na sekta hii yalifikia dola za Marekani million 2 na laki 6 “amesema
Amesema sekta hiyo ilichangia asilimia 17 ya pato la Taifa kwa asilimia 25 ya fedha za kigeni na asilimia 60 ya mapato yatokanayo na biashara na huduma.

Vile vile ameeleza kuwa sekta ya Utalii uzalisha ajira takribani millioni 1 na laki 5 ambazo niajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja .

Amesema kupitia mafunzo hayo yaliotolewa kwa waandishi wa habari yatasaidia kuleta mabadiliko makubwa katika matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika kutagaza vivutuo vya ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo amesema ipo ya kuendelea kutoa elimu ya Utalii zaidi katika jamii ili iweze kujua nini maana ya utalii.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji huyo aliwataka wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa huduma za Utalii kuhakikisha zinakuwa za viwango ili kuweza kuwavutia zaidi watalii wanaokuja nchini

Awali Rais wa TAMPA Simon Mkina amesema kupitia mafunzo hayo wanahabari wamejengewa uwezo wa masuala mbalimbali yanayohusu Utalii ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakileta tija kwa taifa.

“Tanzania Kuna vivutio vingi vya Utalii lakini baadhi yake avielezeki kwa uzuri zaidi na avieleweki kwa watu wengi wa ndani na nje ya nchi hivyo sisi Kama Chama tumeona ni vema kushirikiana na chuo Cha Utalii kuwanoa waandishi ili waweze kujua namna nzuri ya kutagaza Utalii

Na kuongeza kuwa “
kuongezeka kwa Utalii ni kuongezeka kwa mapato ya nchi ambapo fedha ambazo upatikana usaidia kufanya miradi ya maendeleo”amesema Mkina

Kwa upande wake mmoja ya mkufuzi katika mafunzo hayo kutoka Chuo Cha Taifa Cha Utalii Amiri Abdi amesema waandishi was habari ni watu muhimu hivyo kupitia kalamu zao wataipeleka elimu hiyo kwa jamii.