Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MKUU wa sehemu ya Maendeleo ya Mkonge kutoka Bodi ya Mkonge nchini (TSB) Saimon Kibasa amesema,Bodi hiyo kwa kusrikiana na Wizara ya Kilimo imeweka mpango wa kuweka vituo vya usindikaji wa zao la mkonge lengo likiwa ni kumsaidia mkulima mdogo ili aweze kusindika na kupata nyuzi, singa ambazo zitakubalika katika soko la ndani na nje ya nchi.
Akizungumza jijini Dodoma kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji yanayoendelea kwenye viwanja vya Nane Nane jijini Dodoma Kibasa amesema, Bodi imekuwa ikiwaunganisha wakulima na masoko na kwamba sehemu ya masoko hayo ni kuwaunganisha wakulima hao ili wapate soko la bei nzuri.
“Nchini Tanzania wakulima wamegawanyika katika makundi matatu wadogo, wakubwa na wakati huku akisema wakulima wakubwa hawana changamoto kama ilivyo kwa wakulima hao wadogo,
“Na wakulima wadogo nao wamegawanyika katika sehemu mbili wanaolima kwenye mashamba yao binafisi na wanaofanyabiashara lakini wapo ambao wanalima kilimo cha mkataba kinachoendeshwa katika mashamba matano nchini yakiwamo Ngombezi na magoma,” amesema.
Bodi hiyo ni Taasisi ya serikali ambayo ipo chini wizara ya kilimo ni msimamizi na mhamasishaji maendeleo ya mkonge nchini.
Kwa mujibu wa Kibasa , katika mashamba hayo yana mikataba kati ya mkulima mdogo na Bodi ambapo inamkodisha mkulima huyo na kazi yake ni kulima na kutunza mkonge na kwamba kuna mkataba kati ya vyama vya ushirika vilivyopo katika mashamba hayo na usindikaji.
“Amesema,wote hao wanasimamiwa na Bodi kwa kushirikiana na ofisi ya Msajili wa vyama vya ushirika Mkoa wa Tanga katika maeneo hayo TSB imekuwa ikiwasimamia wakulima kuhakikisha wanapata bei nzuri kupitia wanunuzi mbalimbali.”
Kibasa ameongeza kuwa lengo la kuhamasisha kilimo hicho ni zao ambalo lina soko kubwa na ni zao ambalo linastamili magonjwa, ukame na ni la uhakika kumpatia mkulima kipato.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria