March 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TRC yakamilisha majaribio ya mabehewa ya mizigo ya SGR

Na Mwandishi wetu, Timesmajira


Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeutaarifu Umma kuhusu kukamilika kwa majaribio ya mabehewa 264 ya mizigo, yaliyowasili nchini Desemba 2024. Majaribio ya mabehewa hayo yaliyochukua mwezi mmoja yalifanyika chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), yalijikita katika maeneo mawili ambayo ni tuli (static) na mwendo (dynamic).

Taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano,Fredy Mwanjala imesema lengo la majaribio hayo ilikuwa ni kuangalia umadhubuti wa mabehewa treni inapokuwa kwenye mwendo.

Ameaema wakati wa zoezi hilo LATRA imefanya kaguzi za mabehewa yote 264 kati ya hayo 200 yakiwa ni ya makasha (containers carriers) na 64 ni ya mizigo isiyofungwa (loose cargoes).

Aidha,amesema LATRA imejiridhisha kuwa ubunifu wa mwendokasi (design speed) wa kilometa 120 kwa saa umefikiwa na kuthibitisha kuwa yamefanya vizuri katika mifumo yote muhimu ikiwemo breki na kwenye kona (curve). Katika hatua nyingine LATRA imesema itatoa ithibati kwa TRC, kama Sheria na Kanuni zinavyoeleza ili mabehewa haya yaanze kubeba na kusafirisha mizigo.


Kukamilika kwa majaribio ya mabehewa 264 kati ya 1,430 yanayotengenezwa na kampuni va
CRRC ya China, ni kiashiria kuwa usafirishaji mizigo katika reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) uko mbioni kuanza.