Na Rose Itono, Timesmajira
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuanzishwa kwa Mfumo wa matumizi ya Kidigitali umekuwa na muitikiio mkubwa kwa wateja nchini na kuondoa usumbufu wa vishoka.
Akizungumzia hilo leo, kwenye semina ya kuwajengea uwezo wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari Dar es Salaam (DCPC), kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa Kodi Richard Kayombo amesema, Mfumo wa zamani ulikuwa na changamoto nyingi kwa wateja ikiwepo msongamano.
Kayombo Amesema kabla ya TRA kuanzishwa Mfumo huu, vishoka walikuwa wakiwasumbua wateja ikiwa ni pamoja na kuwachukulia fedha zao bila sababu za msingi.
“TRA bado tunaendelea kukusanya maoni Ili kuboresha huduma,”amesema Kayombo na kuongeza kuwa mamlaka imejiwekea lengo la kukusanya jumla ya sh. Tirion 23.1 kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka huu.
Amesema, TRA imekuwa ikifanya semina za aina hii kwenye makundi mbalimbali ili kuwajengea uelewa kuhakikisha elimu ya mlipa kodi inaeleweka.
“Elimu ya Kodi kila siku ina jambo jipya hivyo ni muhimu kila mmoja kilitambua, kama jambo ambalo mamlaka imekuwa ikifanya.
Kwa upande wake, Ofisa Mkuu wa Usimamizi wa Kodi Hamad Mterry amesema suala la kukagua risiti halikwepeki
Hata hivyo, ametaja majukumu ya msingi kwa mamlaka kuwa ni pamoja na kukadiria, kukusanya na kuhasibu Mapato ya serikali kuu kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.
Majukumu mengine ni kukusanya na kuratibu sheria za mapato na kuhakikisha usimamizi ulio wa haki thabiti na madhubuti wa Sheria zote za Mapato zilizopo chini ya Idara za mapato za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, amesema TRA pia ina jukumu la kumshauri Waziri wa Fedha pamoja na Idara nyingine muhimu za serikali Juu ya mambo yanayohusu kodi.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu