Na Joyce Kasiki,Tinesmajira online,Dodoma
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Juma Mwenda amesema, Mamlaka hiyo imejipanga kutatua kero za kikodi kwa wananchi waliokutana na changamoto mbalimbali.
Aidha amewataka wananchi waliofikia kiwango cha kulipa kodi , wafike katika banda la TRA kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji (88) Nzuguni jijini Dodoma ili wapatiwe elimu ya kodi, mabadiliko ya sheria na kufanyiwa makadirio ya kodi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la TRA kwenye maonesho hayo,Mwenda amesema ,wamelenga kutumia fursa ya maonesho hayo kutatua kwa haraka changamoto za wadau wao ambao ni walipa kodi.
“Wadau wengi hutembelea maonesho haya,nasi tumejipanga ,pamoja na mambo mengine kutumia fursa ya maonesho haya ,kutatua changamoto mbalimbali za kikodi wanazokutana nazo wananchi.”amesema Mwenda
Mwenda amewaasa wadau na wananchi kwa ujumla kufika katika banda la TRA ili waweze kupata elimu ya kikodi lakini pia kutatuliwa changamoto mbalimbali za kikodi wanazokabiliana nazo ili zipatiwe ufumbuzi.
Amesema,katika bands la TRA kuna maafisa wao ambao wapo tayari kuwahudumia wananchi kwa kike wanachokihitaji kuhusiana na masuala ya kikodi.
Pia amesema TRA imejipanga kuhudumia walipa kodi kwa haraka ili waweze kuchangia ns hivyo kuwezesha Serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.
More Stories
Mawakili Tabora walaani kuziwa kutekeleza majukumu
RC Mrindoko:Ufyekaji wa mahindi Tanganyika si maelekezo ya serikali
Walimu S/ Sekondari Ilala wafundwa juu ya maadili ya wanafunzi