June 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TPTC kuendesha kozi ya Walinda Amani wa Kirai

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

CHUO cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania (Tanzania Peacekeeping Training Centre -TPTC) kitaendesha  rasmi kozi ya Walinda  Amani wa Kirai ya  Umoja wa Mataifa kwa Nations Development Programme -UNDP na Serikali ya  Japan.

Kozi hiyo itaendeshwa katika ukumbi wa Chuo hicho,Kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam  kuanzia Juni 9 hadi 13 mwaka huu.

Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Chuo cha TPTC,Brigedia Jenerali George Itang’are amesema kwa mara ya kwanza Chuo chao kimezindua rasmi Kozi Maalum ya Mafunzo ya Kiraia katika Operesheni za Kulinda Amani.

Amesema washiriki wa kozi hiyo ni wale wenye sifa ya kuhudumu katika Ulinzi wa amani kutoka Taasisi mbalimbali za Kirai (Civilian Component).

“Lengo la kozi hiyo ni kuwaandaa na kuwawezesha raia hao kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi wanapokuwa kwenye jukumu la ulinzi wa amani,”amesema

Kwa upande wake  Balozi wa Japan nchini Tanzania,Nomura Hiroyuki alisema wanaamini kuwa kuimarisha uwezo wa kulinda amani kupitia ushirikiano wa kimataifa ni hatua muhimu katika kujenga mustakabali ulio imara na salama zaidi.

Amesema Japan itaendelea kujitolea kushirikiana kwa ukaribu na Tanzania pamoja na UNDP ili kuunga mkono juhudi za kudumisha amani Duniani.

Naye Mratibu wa Programu za Utawala Bora kutoka UNDP,Godfrey Mulisa amesema kozi hiyo ni ya kihistoria na inalenga kukuza uwezo wa kiraia kushiriki kikamilifu katika juhudi za kulinda amani ndani na nje ya nchi.

Amesema kwa msaada wa Serikali ya Japan na utekelezaji wa UNDP kwa kushirikiana na kituo hicho kwa kutoa mafunzo ambayo yanajumuishe raia,kundi ambalo ni muhimu na mara nyingi usahaulika katika operesheni za amani.