November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TPLB yafungia uwanja wa Gwambina

Na Mwandishi Wetu

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kuufungia Uwanja wa Gwambina kutumika kuchezewa mechi zozote za mashindano kutokana na eneo lake la kuchezea (pitch) kutokidhi viwango vilivyoainishwa kikanuni.

Uwanja huo umefingiwa saa chache baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya wenyeji Gwambina dhidi ya Kagera sugar na kusalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Hata kabla ya Bodi la Ligi kutangaza kuufundia uwanja huo, tayari kulikuwa na manunguniko kutoka kwa wadau wengi wa soka ambao walikuwa wakifuatilia mchezo huo wakidai hali ya uwanja imewafanya wachezaji wa timu zote mbili kucheza soka lililo la kuvutia kwani kile ambecho walikiona kwa wachezaji hao katika mechi za kwanza za Ligi walishindwa kukiona.

Kutokana na uamuzi ya kufungia uwanja huo, TPLB imeitaka Gwambina kupendekeza jina la uwanja mwingine kati ya CCM Kirumba au Nyamagana vyote vya jijini Mwanza ambao utatumika kwa ajili ya mechi zao za nyumbani za Ligi.

Itakumbukwa kuwa wakati timu hiyo imepanda daraja, uongozi wa timu hiyo uliweka wazi kuwa hawatakuwa na sababu za kuhama katika uwanja huo kwani upo katika kiwango bora na ni miongoni mwa viwanja ambavyo vinaingiza idadi kubwa ya mashabiki.