December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TPHA yasajili viwatilifu 409, Kampuni 198

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Mamlaka ya afya ya mimea na viwatilifu TPHA imefanikiwa kusajili viwatilifu vipya 409 pamoja na Kampuni 198 Kwa kipindi cha 2022 Hadi April 2023

Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi wa TPHA Dkt Joseph Nduguru wakati akiongea na vyombo vya habari wiki iliyopita kwenye maazimisho ya siku ya afya ya mimea ambayo yalifanyika Mei 12 Jijini Arusha

Dkt Ndunguru alisema kuwa usajili wa viwatilifu hivyo ni jitiada ambazo zinafanywa na mamlaka hiyo ambapo lengo halisi ni kuhakikisha kuwa wanalinda na kuboresha afya ya mimea

Aliongeza kuwa mbali na kuweza kusajili viwatilifu hivyo vipya pia wao kama mamlaka wameweza kushirikiana na taasisi nyingine kwa kukusanya sampuli za udongo Kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali

“Tumeahirikiana na taasisi nyingine na tumefanikiaha kukusanya sampuli za udongo 1300 sanjari na kutoa ushauri wa aina ya udongo ambao unaweza kutumika katika matumizi mbalimbali”aliongeza

Katika hatua nyingine alisema wanajivunia kuweza kukusanya sampuli hai 407 na mpaka sasa zipo katika maabara ya Benki ya mimea ya TPHA.

“Mamlaka imefanikiwa kuanzisha pia Benki za asili ambazo Kwa Sasa hizi Benki zipo Karatu na ni Kwa ajili ya mazao kama vile Migomba,miwa, pamoja na Viazi”alisema

Wana habari mkoa wa Arusha wakiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wa TPHA kwenye maazimisho ya siku ya afya ya mimea duniani