January 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TPA yailaza NEMC kibabe michuano SHIMUTA

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Timu ya mpira wa miguu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeendeleza ubabe katika mchezo wa soka kwenye michuano inayoendelea ya SHIMMUTA baada ya kuibugiza timu ya mpira wa miguu ya Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) mabao 4-0.

Katika mchezo huo uliofanyika katika viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), timu ya TPA ilitandaza kabumbu safi na kuwazidi wapinzani katika kila eneo.

Hadi dakika 90 zinamalizika, TPA iliibuka na ushindi wa mabao 4 – 0 yaliyowekwa kimiani na Said Jambae, Shafii Rajabu, Saidi Singano na John Chiwonda.

Huo ni mchezo wa pili kwa timu ya mpira wa miguu ya TPA kuibuka na ushindi. Katika mchezo wa kwanza TPA iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa goli lililofungwa na Ramadhani Madebe
katika dakika ya 10
Ya mchezo.

Matukio mbalimbali katika picha