Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetangazwa kuwa mshindi wa jumla katika michezo ya SHIMMUTA 2023 iliyomalizika jana usiku katika Viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
Akiongea na waandishi wa Habari baada kutangazwa mshindi wa jumla wakati wa shehere za kilele cha michezo hiyo, Meneja Rasilimali Watu wa TPA, Mussa Saidi Msabimana amesema mafanikio hayo yametokana na maandalizi mazuri yalifanywa na timu za TPA kwa ajili ya michuano hiyo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye shehere hizo aliipongeza TPA kwa mafanikio hayo na kuzitaka taasisi kujipanga kwa ajili ya michezo ya mwakani.
TPA imetwaa ubingwa kwa timu zake za basketball ambayo iliinyuka TRA kwa jumla ya vikapu 66-25 katika mchezo wale wa fainali.
Kwa upande wa netball, TPA ilitwaaa ubingwa huo kwa kuigalagaza timu ya Tanesco kwa vikapu 53-36 huku katika mchezo wa Kamba upande wa wanawake iliishinda timu ya TPDC.
Upande wa mchezo wa Kamba wanaume, TPA iliichapa timu ya TBS na kunyakua ubingwa. Kwenye mchezo wa draft kwa wanawake, Bi Celina Simon alimekuwa mshindi wa tatu na kwenye kukimbia ndani ya magunia TPA imetwaa ubingwa wa kwanza.
Upande wa Riadha mita 100 wanaume, TPA illibuka mshindi wa pili na kupata medali ya fedha. Kwenye mita 200 wanaume imetwaa ushindi wa kwanza.
Riadha mita 400 wanawake, imetwaa ushindi kwa kushika nafasi ya pili huku upande wa wanaume kwa mita 400 imetwaa nafasi ya kwanza.
Kwa upande wa mita 800 wanawake, imetwaa nafasi ya pili huku mita 1,500 wanawake ikitwaaa ushindi wa tatu. Mita 1,500 wanaume imetwaa nafasi ya. Pili. Kwenye mita 5000 wanaume tumepata nafasi ya tatu.
Hivyo basi kwa ushindi wa jumla upande wa riadha wanawake imeshika nafasi ya tatu huku mshindi wa jumla wanaume imeshika nafasi ya kwanza. Na upande wa wazee riadha imeibuka mshindi wa jumla.
More Stories
Watumishi wa Fahari wafanya Bonanza
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship