Na Mwandishi Wetu, TimesMajira,Online
MAWAZIRI wa Wizara zote nchini wanatarajiwa kukutana kuchambua kwa kina suala la kilio cha wananchi kuhusu tozo mpya za mialama ya simu zilizoanza kutumika wiki iliyopita.
Kikao hicho cha mawaziri kitatanguliwa na kikao kilichoitishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa ajili ya kujadili suala hilo, ambapo kitafanyika kesho.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, akiwa akiambatana na Waziri wa Teknolojia ha Habari na Mawasiliano Dkt. Faustine Ndugulile.
Amesema Serikali imesikia kilio na maoni ya wananchi kuhusu tozo mpya ya miamala ya simu na kuwaomba wawe watulivu wakati jambo hilo linatafutiwa ufumbuzi.
Kwa upande wake Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Dkt. Faustine Ndugulile alibainisha kuwa Wizara yake pia ambayo inaguswa moja kwa moja na tozo hizo imeendelea kupokea maoni na kuchakata taarifa mbalimbali tangu tozo hiyo ianzishwe na kumwahidi Waziri wa Fedha na Mipango kwamba atampa ushirikiano kuhakikisha kwamba maelekezo yaliyotolewa na viongozi yanatekelezwa.
More Stories
Rais Samia afanya uteuzi
Waliombaka, kulawiti binti wa Yombo, Dar jela maisha
BREAKING NEWS: Rais Dkt Samia afanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali usiku huu