January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TotalEnergies yaunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline, Dar

KAMPUNI ya Mafuta ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, imeamua kumuunga mkono Rais Samia, kwenye kampeni ya nishati bora ya kupikia, kwa kuanza kusambaza gesi ya kupikia, katika vituo vyake vyote zaidi ya 100 nchini, ili kufanikisha ndoto ya Rais Samia, kufikia mwaka 2030, Watanzania wote wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Uamuzi huo, umetangazwa na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa Total, Getrude Mpangile, wakati wa siku ya pili ya wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza jana kwa uzinduzi wa kituo cha mafuta cha TotalEnergies Magomeni Makanya, ile njia ya Tandale Uzuri.

Mpangile alisema, kufuatia kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Rais Samia, kuhamasisha matumizi ya nishati salama ya kupikia, kwa vile TotalEnergies, ndio kampuni inayoongoza Tanzania kwa idadi ya vituo vya mafuta, TotalEnergies, imeamua kumuunga mkono Rais Samia kwenye suala la nishati bora ya kupikia, hivyo sasa itasambaza gesi ya majumbani, katika kampeni iitwayo “Jiko Bomba, Pishi Pambe”.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mtandao wa Vituo vya TotalEnergy, Abdul-Rahim Siddique, amezungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu alisema; “Ni siku ya furaha kusherehekea wateja wetu, washirika na hatua muhimu za kampuni katika kuhudumia jamii ya Tanzania kwa bidhaa na huduma za ubora wa juu kutoka TotalEnergies na kwa mdau wetu Mohamed Binzoo ambaye ni muuzaji na mmiliki wa TotalEnergies Makanya Service Station.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Vituo vya mafuta TotalEnergies Abdul Rahim Siddique akizungumza kuhusu namna Kampuni ya TotalEnergies ilivyijipanga kutoa huduma katika kituo hicho wakati wa uzinduzi wa Kituo cha mafuta cha TotalEnergies kilichopo Makanya, Magomeni jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.

Meneja Masoko wa TotalEnergies, Caroline Kwakwezi, amesema Kaulimbiu ya Wiki ya Wateja wa Afrika ya 2024 inavyoendelea “Kukusaidia kila mahali, kila wakati, katika bara zima,” hakuna njia bora ya kuionyesha kuliko kusambaza bidhaa na huduma zetu kwa wakazi wa Makanya Tandale na jumuiya jirani. Hii ndiyo taswira ya matarajio yetu ya kuifikia kila Tanzania bidhaa za ubora wa juu za Excellium, Vilainishi, Kadi, Gesi, Taa za Jua na Huduma kutoka TotalEnergies”,

Katika hotuba yake, mmiliki wa TotalEnergies Makanya Service Station, Thabit Bizoo alitoa shukrani zake kwa kampuni ya TotalEnergies na wateja wao waaminifu kwa mafanikio ya kituo cha huduma cha Makanya, “Nawashukuru sana TotalEnergies kwa msaada wao tangu kujengwa. ya kituo kwa uendeshaji wake wa sasa ambao umetuwezesha kuwa hapa leo katika kituo hiki kizuri.

Shukrani nyingi pia ziwaendee wateja wetu wa Makanya wanaoamini chapa ya TotalEnergies ambayo imewawezesha kutuamini na kuturuhusu kuwahudumia. Tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu ili uwe na matumizi bora zaidi katika Kituo cha Huduma cha TotalEnergies Makanya na ushiriki maoni yako nasi ili tuweze kukuhudumia vyema zaidi.”

Kituo cha TotalEnergies Makanya hutoa nishati bora, urahisi na huduma ya kipekee kwa jamii. Kwa kuzingatia kuridhika kwa wateja na ubora, tunalenga kuwa kivutio kinachopendelewa kwa wateja wanaohitaji mafuta, gesi, vilainishi, taa za jua na vifaa vya huduma kwa wakazi wa Makanya na jumuiya jirani zao. End.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Vituo vya mafuta TotalEnergies Abdulrahim Siddique pamoja na Mkurugenzi wa Kituo cha Mafuta cha TotalEnergies cha Makanya Thabit Amer wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha mafuta cha TotalEnergies cha Makanya ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja

Mkurugenzi wa Mtandao wa Vituo vya mafuta TotalEnergies Abdulrahim Siddique pamoja na Mkurugenzi wa Kituo cha Mafuta cha TotalEnergies cha Makanya Thabit Amer wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha mafuta cha TotalEnergies cha Makanya ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja

Mkurugenzi wa Mtandao wa Vituo vya mafuta TotalEnergies Abdul Rahim Siddique akizungumza kuhusu namna Kampuni ya TotalEnergies ilivyijipanga kutoa huduma katika kituo hicho wakati wa uzinduzi wa Kituo cha mafuta cha TotalEnergies kilichopo Makanya, Magomeni jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.

Mkurugenzi wa Kituo cha Mafuta cha TotalEnergies cha Makanya Thabit Amer akizungumza kuhusu uwekezaji uliofanywa pamoja na nmna watakavyotoa huduma katika kituo hicho wakati wa uzinduzi wa Kituo cha mafuta cha TotalEnergies kilichopo Makanya, Magomeni jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.

Meneja Masoko wa TotalEnergies, Caroline Kakwezi akizungumza kuhusu Kampuni ya TotalEnergies inavyoendelea kufungua njia kwa makampuni mbalimbali kuweza kufungu vituo vya mafuta kwa chapa ya TotalEnergies ili kuweza kutoa huduma iliyobora kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa Kituo cha mafuta cha TotalEnergies kilichopo Makanya, Magomeni jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TotalEnergies pamoja na wadau mbalimbali wa kampuni hiyo wakifuatilia uzinduzi wa Kituo cha mafuta cha TotalEnergies kilichopo Makanya, Magomeni jijini Dar es Salaam