December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TORITA inavyopambana kuhakikisha zao la tumbaku linaongeza tija kiuchumi

Na Joyce Kasiki,Tiesmajira online,Tabora

WAKULIMA wa zao la Tumbaku hapa nchini wametakiwa kuachana  na kilimo ha mazoea na badala yake wafuate maelekezo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Tumbaku Tanzania (TORITA) ili kuongeza tija kwenye uzalishaji kwa ajiliya maslahi yao naTaifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tabora Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TORITA Gration Rwegasira amesema zao la tumbaku ni moja ya zao linalochangia kwa kiasi kikubwa fedha za kigeni na hvyo kuongeza tija katika pato la Taifa.

“Licha ya kutozungumzwa sana lakini tumbaku ni zao linalotajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la Taifa kutokana na fedha za kigeni.”

Aidha amesema ,Bodi ina  jukumu la kuangalia namna TORITA inavyotekeleza majukumu yake ya  msingi ya kutafiti zao la tumbaku kuanzia uzalishaji wa mbegu za ndani ili kuhakikisha mkulima anapata mbegu bora lakini kuepusha fedha nyingi zinazotumika kununua mbegu nje ya nchi.

Prof.Rwegasira amesema tumbaku ni zao la pili linaloiletea nchi fedha za kigeni huku akisema hilo ni zao muhimu sana kwa uchumi wan chi.

Mmea wa tumbaku

“Kwa hiyo sisi tunatamani liendele kupiganiwa ili liweze kusaidia nchi iweze kusonga mbele.”amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TORITA Dkt.Jacob Lisuma amesema,taasisi hiyo ilianzishwa mnamo 2000 ikiwa na malengo ya kufanya tafiti za kuongeza ubora wa zao la tumbaku na zinazohifadhi mazingira kwenye maeneo ya tumbaku .

“Kwa hiyo idara ya tafiti wanaangalia upatikanaji wa mbegu bora zaidi zinazoongeza tija kwa mkulima na kuongeza uzalishaji kwa ujumla ili kuipatia nchi mapato kwani tumbaku inayozalishwa hapa nchini inachakatwa na inakwenda nje ya nchi.”amesema

Kwa mujibu wa Dkt.Lisuma ,teknolojia zinaopatikana katika taasisi hiyo ya utafiti zinachukuliwa na idara ya mafunzo na uenezaji wa teknolojia kwenda  kwa wakulima ambapo kwa sasa wanaendelea na uboreshaji wa mbegu aina tano zilizobuniwa na TORITA  ambazo zinapitia mchakato wa mwisho na baadaye zitawalishwa taasisi ya udhibiti wa mbegu Tanzania kwa ajili ya usajili.

MKURUGENZI wa TORIRA Dkt.Jacob Lizuma

Akielezea kuhusu mafanikio tangu uanzishwa kwa taasisi hiyo Dkt.Lisuma amesema kabla ya kuanzishwa TORITA nchi ilikuwa inazalisha kilo milioni 10 hadi milioni 15 lakini walianza kupanda kidogo kidogo na mpaka mwaka huu wameweka makisio ya juu ya kuzalisha kilo milioni 140.

Kuhusu changamoto zinazowakabili amesema ni pamoja na upungufu wa watumishi ,waliopo ni 30 na wanahitaji kuwa na watumishi 61 ili waweze kukamilisha maukumu yao kikamilifu.

Hata hivyo amesema mipango na mikakati ya TORITA ni kuongeza uzalishaji kila mwaka ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuanzishwa kwake.