December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TMDA yatoa Tuzo kwa waandishi wa habari

Na Mwandishi wetu,Iringa

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Nchini (TMDA) kwa mara ya tatu leo imetoka tuzo kwa Waandishi wa habari bora wa Uandishi wa habari za dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa za tumbaku.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo ambazo pia ziliambatana na Kikao kazi Cha Wahariri na Waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba, Sura 219 iliyofanyika Mkoani Iringa, Dkt.Adam Fimbo amewapongeza waandishi walioibuka washindi huku akiwasisitiza wandishi kuendelea kuandika habari za TMDA zenye kuleta tija kwa jamii.

Amesema kuwa tuzo hizo ni sehemu ya jitihada za TMDA wanazozifanya kwa waandishi wa habari katika kuripoti habari za dawa, vifaa tiba, bidhaa za tumbaku na vitendanishi katika kuuhabarisha umma wa watanzania.

“Tunataka mtuandike mambo yote ambayo mmeyachunguza vizuri,yaandikwe ili tujirekebishe ,”amesema na kuongeza

“Tuzo hizi ni maazimio ya kikao kazi yaliyofanyika mkoani Arusha Mwaka 2021 ambapo Mwaka 2022 tulianza utekelezaji wake,”amesema

Aidha amesema utoaji tuzo hizo ni kutambua kazi kubwa inayofanywa na waandishi wa habari katika kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Dawa na vifaa tiba na ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza endapo dawa hizo hazitatumiwa ipasavyo.

Sambamba na hayo amewahimiza waandishi wa habari kuendelea kuelimisha jamii bila kuchoka kwani wana nafasi kubwa ya kuwafikia Wananchi.

Waandishi walioshinda tuzo hizo nafasi ya kwanza ni Veronica Mrema kutoka blogu ya Matukio na Maisha, , wapili Madina Mohammed kutoka blogu ya Wamachinga Tv ,Mshindi wa Tatu, Penina Malundo kutoka blogu ya Times Majira , huku mshindi wa nne akiwa ni Andrew Chale wa Matukio Daima.