April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TMDA yakamata Dawa zisizo na usajili

Na Mwandishi wetu, timesmajira,Dar es Salaam

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imekamata dawa ambazo hazijasajiliwa zenye thamani ya TSh 294,486,590 milioni ambapo tozo yake inakaribia kuwa  Milioni 80 zimekamatwa  kufuatia ukaguzi maalum,   uliofanyika eneo la Mtaa wa Kitumbini katika Kata ya Mchafukoge katikakati ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza katika eneo la tukio, Meneja wa Kanda wa TMDA, Adonis Bitegeko amesema timu ya TMDA ya  Kanda ya Mashariki, imekamata  ghala bubu ambalo halijasajiliwa na TMDA, ambapo limebainika ghala hilo  lipo chini ya mmiliki wake Amaiya Rijendra likiwa limehifadhi dawa mbalimbali za binadamu ambazo hazijasajiliwa.

Amesema walifanikiwa kuwasiliana na Jeshi la Polisi   na kumchukua mtuhumiwa kwaajili ya hatua zaidi  za kisheria na TMDA tumekusanya dawa zote ambazo hazijasajiliwa na kuzichukua.”Tumechukua   taratibu za kuziorodhesha na hatua kadhaa za kisheria ikiwemo kuwatoza faini na pia watatakiwa kulipia gharama za kuziteketeza”,amesema 

Aidha, TMDA ilitoa onyo kwa wanaoendelea kufanya biashara hiyo haramu kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria ambapo pia amewaonya pia wataalamu husika wanaojihusisha na biashara hizo haramu kuwa hawatosita kuwafutia leseni zao  za kitaaluma.

Ametaja dawa hizo  zilizokamatwa kuwa ni pamoja na Dawa za magonjwa ya shinikizo la damu, dawa za kutoa ujauzito na  dawa nyingine tofautitofauti.

Mtuhumiwa aliyekutwa nazo ni mtanzania mwenye asili ya India ambapo alipohojiwa alikiri kuendesha ghala hilo bubu pasipo na kibari na kinyume na sheria kwa kile alichodai hakufahamu mamlaka husika za usajili,