NA Penina Malundo,Timesmajira
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imefungua kituo cha kufanya uchunguzi wa awali wa sampuli za dawa za kutibu magonjwa ya kipaumbele ikiwemo malaria, kifua kikuu na makali ya virusi vya ukimwi kwa kutumia Maabara Hamishika ( MIN LAB KIT) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu tarehe 11 Novemba, 2024.
Katika tukio hilo Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa Mashariki,Sophia Mziray ameweza kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Kenan Kihongosi maabara hamishika hiyo yenye thamani ya takribani shilingi Milioni 40.
Awali Meneja huyo wa Kanda amebainisha kuwa, Faida za kuwa na Maabara hiyo itarahisisha uchunguzi wa sampuli za dawa kutoka katika soko kwa eneo hilo na hivyo kuendelea kuwahakikishia wananchi ubora, usalama na ufanisi wa dawa nchini na hivyo kulinda afya ya jamii.
Aidha, Katika tukio hilo pia limeshuhudiwa na watendaji mbalimbali wakiwemo Katibu Tawala Prisca Kayombo, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface na Mganga Mfawidhi hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Dkt. Ndabakubi.
More Stories
Rais Samia kuandika rekodi mkutano G20
Waziri Lukuvi aeleza maono ya Isimani ijayo
Madiwani Korogwe TC wahakikishiwa maji ya uhakika