Na Penina Malundo,Timesmajira
TATIZO la dawa na vifaa tiba bandia lipo katika nchi zote duniani ikiwa ni pamoja na nchi zilizoendelea ambapo ni tatizo la uhalifu unaovuka mipaka ya nchi moja kwenda nchi nyingine (cross border crime).
Nchini Tanzania tatizo hili linaendelea kudhibitiwa na mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ambapo imekuwa mbele kuhakikisha dawa hizo au vifaa hivyo havipati muda wa kuingia nchini.
Mikakati na mipango mbalimbali imekuwa ikipangwa na TMDA katika kudhibiti uingiaji huo wa dawa bandia na vifaa tiba ambavyo vinakuwa na madhara makubwa kwa watumiaji.
Miongoni mwa mikakati iliyowekwa na TMDA ni kuhakikisha inatoe elimu mbalimbali kwa wananchi pamoja na waagizaji na wafanyabiashara wa bidhaa za tiba katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Na miongoni mwa elimu wanayoitoa ni pamoja na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara hao na waingizaji dawa nchini na kukumbushana ufatwaji wa sheria,kanuni na miongozo ya TMDA katika uingizwaji wa dawa nchini.
Pia TMDA imeendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha dawa hizo na vifaa tiba vinazuiliwa kuingia nchini hususani katika maeneo ya mipaka na viapogundulika hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi ya watakaobainika.

Dkt.Yonah Mwalwisi,Mkurugenzi, Udhibiti wa Dawa kutoka TMDA,anasema upatikanaji wa dawa bandia na duni nchini upo chini ya asilimia moja ambapo bado kuna utumiaji wa dawa bila kufata maelekezo ya Daktari kwa baadhi ya watu.
Anasema katika udhibiti wa dawa hizo ufanyiwa tathmini na usajili wa bidhaa tiba ni lazima utumie mfumo wa kieletroniki ambapo ni lazima mteja awasilishe ombi la usajili(dossier)ili tathmini iweze kufanyika.
Anasema tathimini hiyo mara nyingi ufanywa na watathmini waliobobea kwa hatua mbalimbali ikiwemo kukagua Kiwanda kinachotengeneza dawa hizo.
Dkt. Malwisi anasema jumla ya bidhaa tiba 5983 zimesajiliwa nchini kwa kipindi cha mwaka 2019/20 hadi 2022/22.”TMDA ilipokea idadi ya maombi ya vibali vya kuingiza bidhaa tiba nchini takribani 21,557(21,934)kwa mwaka 2019/20 na kwa mwaka 2022/23 ni 4,956(5,334).
”Idadi hii imekuwa ikiongezeka kila mwaka kutokana na uwepo wa mazingira mazuri ya uingizwaji dawa nchini kwa kufata sheria na taratibu mbalimbali zilizowekwa katika vifungu vya sheria,”anasema
Anasema ili dawa iingie nchini,mfumo wa kielektroniki hutumika katika kukagua na ili bidhaa ingizwe nchini lazima iwe imesajiliwa.
Malwisi anasema kibali cha dawa kinaweza kutolewa pia kwazisizosajiliwa kwa maslahi ya nchi baada yakukidhi vigezo vya ubora na vingine huwezesha ukaguzi wa bidhaa tiba zinazoingizwa nchini kupitia vituo vyaforodha rasmi 16 nchi nzima.
Anataja vituo hivyo vya forodha ni pamoja na kituo cha Julius Nyerere International Airport (JNIA),Dar es Salaam Sea Port, KilimanjaroInternational Airport, Horohoro, Holili,Namanga, Sirari, Mwanza Lake Port,Mwanza Airport, Tanga Sea Port, Tunduma, Mtukula, Rusumo, Manyovu, Kasumulo na Kabanga.
*** Akizungumzia ufatiliaji wa ubora.Malwisi anasema ufatiliaji wa ubora wa bidhaa tiba katika soko ufanyika kwa bidhaa tiba na kuruhusu kuwa sokoni .
Anasema ufatiliaji huo huhisisha na utaratibu wa uchukuaji wa sampuli kutoka sokoni na kisha kuzifanyia uchunguzi wa kimaabara ambapo utaratibu huo ulianza tangu mwaka 2009.
***Akizungumzia umuhimu wa utumiaji dawa sahihiDkt. Malwisi anataja miongoni mwa dawa ambazo asilimia upenda kutumia dawa hizo bila maelekezo ni pamoja na zile za kuongeza nguvu za kiume na za utoaji wa mimba.
”Kuna umuhimu wa kutumia dawa kwa usahihi hivyo TMDA imekuwa ikitumia matakwa ya sheria na masharti kwa dawa zote.”Ni matarajio yetu elimu tunayoendelea kutoa kwa jamii itasaidia kwenye mapambano ya udhibiti wa bidhaa bandia na duni ,”anasema.
More Stories
Sakaya;Mungu,ujasiri na kujiamini ndio siri ya mafanikio safari ya siasa/ kutetea wananchi-sehemu ya mwisho
Sakaya:Mungu,ujasiri na kujiamini ndio siri ya mafanikio safari ya siasa/ kutetea wananchi-sehemu ya kwanza
Wakazi mabogini waomba mabadiliko ya Sheria kurahisisha upatikanaji haki kwa waathirika wa ukatili