January 26, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TMB yawataka vijana wenye vipaji kuchangamkia fursa

Na Bakari Lulela,TimesMajira Online

TAASISI ya TMB Family ya jijini Dar es Salaam imewataka vijana wenye vipaji kuchangamkia fursa mbalimbali zitolewazo na taasisi hiyo kama azma ya kuinua na kutimiza malengo yao ikiwemo kupunguza changamoto za ajira zinazoikabili jamii.

Akizungumza katika hafla maalumu, msemaji wa taasisi hiyo Saleh Nassoro amesema TMB wamekuwa wakiwasapoti vijana wenye vipaji vya muziki, Uchoraji, Vinyozi na saluni kwa akina dada kufikia malengo yao.

“Kupitia kipaji changu cha kinyozi masuala ya fashion nimeweza kuwasaidia wasanii wa muziki wa bongo fleva na naendelea kuwashika mkono kuweza kushiriki katika kutimiza azma ya kubuni mavazi ya wasanii sambamba na unyoaji wa mitindo mbalimbali ya nywele,” amesema Nassoro.

Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi hiyo Rijay Ayubu amesema, kupitia Cutting master yake ameweza kuwapatia vijana ajira na kuendelea kufungua fursa mbalimbali za kuwafanya kundi hilo kuwa wenye kufanyakazi ndani ya jamii.

Mkuu huyo amewataka vijana kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuliendeleza Taifa lenye nguvu kazi ya kutosha kiasi ambacho kufanya ongezeko la uchumi wa nchi kuweza kupanda kutokana na rasilimali watu ikiwemo vijana kutokuwa tegemezi.

Mkurugenzi huyo amedai kufanya uzinduzi wa huduma zake za saluni kwa upande wa VIP kama njia ya uboreshaji wa sekta hiyo kwa kuwahudumia watu wa aina zote ikiwemo viongozi, wasanii na wengine wa kipato cha kati.