May 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TMA yatoa utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imesema hali ya hewa kwa saa 24 zijazo baadhi ya mikoa inatazamiwa kuwa na vipindi vya upepo mkali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TMA vipindi vya upepo mkali vinatazamiwa katika maeneo ya mikoa ya Pwani ya Bahari ya Hindi,Lindi,Mtwara, Tanga,Dar es Salaam ikijumuisha Visiwa vya Mafia,Unguja na Pemba .

Aidha kwa mujibu wa TMA tahadhari nyingine ya vipindi vya upepo mkali imetolea kwa mikoa ya Ukanda wa Ziwa Nyasa ,Mikoa ya Njombe ,Ruvuma na Mbeya pamoja na mikoa ya Ukanda wa Kusini mwa mikoa ya ziwa Tanganyika, Mikoa ya Katavi na Rukwa.