Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imetoa taarifa ya uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa hali ya joto,upepo na mvua katika msimu wa Juni hadi Agosti 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa TMA na makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi Dkt.Ladslaus Changa amesema
Ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kawaida kwa kipindi cha juni hadi Agosti,JJA utawaliwa na hali ya baridi .
Dkt.Changa amesema katika kipindi hicho maeneo mbalimbali ya nchi utawaliwa na baridi na upepo mkali kwa maeneo mengi ya nchi yetu na muhtasari, mwelekeo wa msimu wa JJA 2025 .
“TMA yatoa mwelekeo wa msimu wa Kipupwe Juni mpaka mwezi Agosti ambapo kwa kawaida, kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti (JJA), hutawaliwa na hali ya baridi na upepo mkali kwa maeneo mengi ya nchi, kwa muhtasari, mwelekeo wa msimu wa JJA, 2025 unaonesha kuwa na hali ya joto alisema Dkt, Ladslaus.
Dkt.Changa amesema hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi hata hivyo, hali ya baridi ya wastani hadi baridi kali inatarajiwa katika maeneo ya mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Singida pamoja na maeneo ya magharibi mwa mkoa wa Dodoma.
Aidha amesema vipindi vya baridi zaidi vinatarajiwa kujitokeza katika mwezi Julai na vipindi vya mvua za nje ya msimu vinatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria, ukanda wa mwambao wa pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Amesema msimu wa kipupwe 2025 unatarajiwa kutawaliwa na upepo wa wastani utakaovuma kutoka kusini Mashariki kwa maeneo mengi ya nchi, na vipindi vichache vya upepo mkali utakaovuma kutoka kusini (upepo wa kusi) hususan katika kipindi cha miezi ya Juni na Julai 2025 katika maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi na maeneo ya nchi kavu.
Amesema magonjwa yanayohusiana na hali ya hewa ya baridi kama vile homa ya mapafu na magonjwa ya mifugo yanaweza kujitokeza, ingawa kwa kiasi kidogo.
More Stories
FMF:Taifa bado linahitaji elimu masuala ya afya ya uzazi
Dkt.Tax:Vyombo vya usalama vinaendelea kuchukua tahadhari ,Taifa lipo salama
JAB yatoa mwezi mmoja kwa waandishi wa habari kujisajili mfumo wa Tai -Habari