December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TLS wafanya uchaguzi na kutangaza matokeo waliowania nafasi za Chama

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Chama Cha mawakili Tanganyika (TlS) kimefanikiwa kufanya uchaguzi na kutangaza matokeo ya  viongozi wa waliowania nafasi mbali mbali katika Chama hicho 

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo  uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa AICC mkoani Arusha  mwenyekiti wa kamati  ya uchaguzi Charles Rwechungura amemtangaza mshindi wa nafasi ya urasi katika Chama hicho 2022-2023 kuwa ni profesa Edward Hosea aliyeshinda kwa kukura  621

 Nafasi ya urasi ilikuwa ikiwaniwa na wagombea wa 3 ambapo jumla ya kura zilizo pigwa ni 1150 na wagombea walikuwa wakiwania nafasi hiyo ni harodi sungusia aliyepata  380 ,Jeremiah mtopesa kura 145 , na profesa Edward Hosea aliyepata kura  621

Akizungumza Mara baada ya matokeo ya uchugzi huo  Raisi wa chama Cha mawakili Tanganyika (Tls) Profesa Edward Hosea amesema katika  awamu ya pili ya uongozi wake kutakuwa na  uwazi na  uwajibikaj kwa mawakili .

Awali mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Charles Rwechungura aliwatangazi washindi wa nafasi mbali mbali waliogombea ndani ya chama hicho ikiwemo nafasi ya mwakilishi, mwenyekiti wa vijana mawakili pamoja na Makamu wa Raisi 

Hata hivyo viongozi wote walioshinda nafasi mbali mbali ndani ya chama Cha mawakili Tanganyika (Tls) waliapishwa na kukabidhiwa majukumu yao rasmi