November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TIRA:Wakulima,wafugaji,wavuvi wekeni bima ya uwekezaji wenu

Na Joyce Kasiki,Dodoma

MAMLAKA ya Bima Tanzania imewaasa wananchi wajifunze na watumie bidhaa za Bima za kilimo,ufugaji na uvuvi ili waweze kujilinda dhidi ya majanga.

Hatua hiyo itamwezesha mkulima,mfugaji na mvuvi kulinda uwekezaji wao kwa kufidiwa pindi yanapotokea majanga.

Kamishna wa Bima Tanzania Dkt.Baghayo Saqware ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kilele cha cha maadhimisho ya siku kuu ya wakulima,wafugaji na wavuvi (Nane nane ) katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

“Bidhaa za bima husaidia muhusika kufidiwa pindi yanapotokea majanga yatokanayo na mafuriko,wadudu waharibifu,ukame ,majanga ya moto kwenye mashamba na kuharibu mazao ,yote hayo yanalipwa na kampuni za Bima.” Amesema

Ameongeza kuwa “Kwa hiyo tunawasihi wakulima ,wafugaji na wavuvi waje wakate bima .”amesema Saqware

Dkt.Saqware amesema kuwa katika sekta hizo watu wamekuwa wakitumia fedha nyingi kufanya uwekezaji huku akisema uwekezaji huo unatakiwa ulindwe kwa bima.

“Ukikata Bima uwekezaji wako wote uliowekeza kwa fedha nyingi unalindwa kwa gharama kidogo na bima ,