December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Timu ya Mahakama bingwa mpira wa miguu dhidi ya timu ya Bunge,CRDB  Bunge Grand Bonanza

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

BONANZA  la CRDB  Bunge Grand Bonanza lafanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma,Juni 22,2024 likishirikisha Taasisi mbalimbali pamoja na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ambapo Timu ya Mahakama ya Tanzania iliyohusisha majaji,Mahakimu imeibuka mshindi katika michezo wa mpira wa miguu iliyocheza dhidi ya Timu Bunge la Tanzania katika mashindano ya Bunge Grand Bonanza baada ya mchuano mkali wa dakika 90 ulihitimisha kwa bao moja kwa moja na baadae mahakama kunyakua ushindi kwa mikwaju ya penati ya goli nne kwa tatu.

Bonanza hilo limeshuhudiwa na Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar,Hemed Suleiman Abdulla ambaye amemwakilisha Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Ally Mwinyi.

Amelipongeza Bunge la Tanzania pamoja na Benki ya CRDB kwa kuja na Bonanza hilo kwakuwa siyo tu ushirikiano bali linajenga afya za washiriki.

Naye spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU),Dkt. Tulia Ackson amesema kwamba lengo la Bonanza hilo ni kujenga mahusiano kati ya watumishi wa Bunge pamoja na taasisi zingine.

“Sambamba na kujenga afya lakini lengo la Bonanza hili ni ushirikiano kati yetu na wadau,”amesema.

Katika bonanza hilo michezo mbalimbali ilichezwa ikiwemo mpira wa miguu,mpira wa pete,kufukuza kuku ,kupokezana vijiti kula chakula, kunywa soda, kukimbia na magunia,mbio za riadha na michezo mingine.

Aidha bonanza hilo lilihudhuriwa  na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko Mkuu wa Mkoa wa Dodoma RosemarySenyamule,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri.

Dhumuni kuu la bonanza hilo ni kuwezesha ujenzi wa sekondari ya wavulana (Bunge Boys),kujenga afya pamoja na kuimarisha ushirikiano na taasisi mbalimbali.