Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Tigo Tanzania leo imewazawadia kundi la pili la wateja 20 wa Tigo Pesa milioni 40/- kama sehemu ya promosheni inayoendelea ya Mwaa Mwii.
Washindi hawa walichaguliwa kutoka kwa sampuli nasibu za wateja waliobahatika wa Tigo Pesa ambao walifanya miamala tofauti kama vile Lipa Kwa Simu, Bill Pay, On net P2P, IOP kupokea wiki inayoishia tarehe 27 Machi 2022.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa Kitengo cha Wateja wa Thamani ya Juu wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema,
“Tunajivunia kuwazawadia washindi 20 kwa kundi letu la pili la 2m/- kila mmoja, hadi sasa tumetoa zaidi ya 80m/-, na kimahesabu kutoka katika jumla ya 325m/, 245m/- bado zinaendelea kuchukuliwa, hivyo tunawaomba wateja waendelee kufanya miamala yao kupitia Tigo Pesa”.
“Promosheni hii ya wiki 6 ni maalum kwa wateja wa Tigo Pesa, ambapo hadi sasa tayari tumeshuhudia washindi 40 wakishinda 2M kwa wiki 2 za kwanza, washindi 10 kupata zawadi ya mwisho ya 10M ya promosheni na mshindi 1 wa jumla akipata 25M.
Wateja hupata kufanya miamala mingi iwezekanavyo kutoka kwa huduma zilizotajwa hapo juu ili kupata nafasi ya kushinda.” Alieleza Rutta.
Naye mfanyabiashara wa samaki, kutoka Kigamboni jijini Dar es Salaam akiwa katika hali ya shangwe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alisema,
“Ninapenda kumshukuru Mungu kwa fedha hizi ambazo zitanisaidia kununua friji mpya, nilisikia mara moja. redio kuhusu promosheni hii, lakini katika ndoto zangu sikuwahi kujua kuwa nitakuwa miongoni mwa washindi wa wiki hii, ninatumia Tigo Pesa kila siku, hivyo huwezi jua, kwa bahati nzuri naweza pia kuibuka mshindi wa 25m/-”.
Washindi 20 ni pamoja na,
Mteja anachohitaji kufanya ni kufanya miamala mara nyingi awezavyo kupitia huduma za Tigo Pesa (Lipa Kwa Simu, Bill Pay, On net P2P, IOP kupokea) zinazopatikana ili kupata nafasi ya kujishindia zawadi za pesa taslimu zinazotolewa.
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19