December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tigo yaboresha mtandao wake kuwasaidia wakulima,wafugaji

KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Mtandao wa Tigo , imesema imeboresha mtandao huo na kuwa mtandao wenye kasi unaoongoza hapa nchini kwa lengo la kuwasaidia wateja wake kufanya shughuli zao zikiwemo za kilimo,uvuvi na ufugaji.

Aidha imeleta simu janja za bei nafuu ili wakulima,wafugaji na wavuvi hata wenye kipato cha hali ya chini waweze kumiliki simu janja na kufanya shughuli zao kimtandao.

Akizungumza katika maonesho ya wakulima na wafugaji ,Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kati Said Iddy amesema kwa kutumia mtandao wa tigo wakulima na wafugaji wanapata fursa ya kutafuta masoko ya bidhaa zao.

Amesema kupitia mtandao wa tigo ulioboreshwa ,wakulima,wafugaji na wavuvi wanakwenda kuoata taarifa za masoko ya bidhaa zao na bidhaa nyingine wanazohitaji ili kuboresha shughuli zao.

Amewaasa wananchi,wakulima,wafugaji na wavuvi kufika kwenye banda la Tigo ili wakajipatie bidhaa za mtandao huo wenye kasi ikkwemo simu janja aina ya ZTE A34 inayopatikana kwa mkopo wa kianzio cha shilingi 35,000.

David Mazuguni mkazi wa Chahwa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambaye alifika katika banda hilo ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwawezesha wananchi wa hali ya chini kumudu kumiliki simu janja.
Xxx

Na Joyce Kasiki,Dodoma

MFUKO wa Pensheni wa Wastaafu (PSSSF) umekuja kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji (88) na mfumo mpya wa PSSSF kidigitali utakaowasaidia wanachama wa mfuko huo kupata huduma mbalimbali za mfuko bila kufika ofisini.

Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF Innocent Sizulwa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Mfuko huo Nzuguni jijini Dodoma.

Sizulwa amesema mfumo huo utawasaidia kupata taarifa zao kwa kwenye simu zao za mkononi kwa.maana ya simu janja .

“Kupitia mfumo huo na kwa kutumia simu janja ,mteja atapata huduma zote ikiwemo taarifa za michango yake ,kusajili mafao,kuongezea taarifa mbalimbali za kiuanachama kama idadi ya watoto na wategemezi katika mfuko.”amesema Sizulwa

Amesema ili kujiunga na katika mtandao huo,mwanachama anapaswa kuwa na namba ya simu,sahihi na namba ya utambulisbo wa Taifa.

“Mfumo huu sasa humwezesha mteja kufanya shughuli za PSSSF akiwa nyumbani.

Kwa upande Rehema Mkamba Afisa Mawasiliano ameaema PSSSF imewekeza kwa wadau kama bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro ambao hutengeneza viatu,mikanda,mikoba na kuuza kwa wateja wao yakiwemo majeshi.

Vike vike ameaema mfuko umewekeza kwenye ranchi za kisasa ya Nguru ya Mvomero