January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tigo wazindua duka jipya la kisasa Palm Village Mall

TimesMajiraOnline

Mtandao namba moja Nchini kwa utoaji wa huduma za Kidigitali Tigo Tanzania wamezindua Duka jipya la kisasa litakalopatikana Palm Village Mall iliyopo kando ya barabara ya Mwai Kibaki Mikocheni, Dar es Salaam ambapo wateja wa Tigo sasa watapata huduma zote za Tigo katika Duka hilo.

Duka la kwanza la aina yake lililoboreshwa kwa njia ya kidijitali litatoa huduma zote zitakazojumuisha ubadilishaji wa SIM, uthibitishaji wa nambari, huduma za Tigo Pesa, huduma za Tigo Business, huduma za usajili wa SIM Card kwa kibayometriki, na skrini za kuonyesha vifaa kwa aina mbalimbali za simu na vifaa zinauzwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Uthmaan Madati amesema uzinduzi wa duka hilo jipya unaenda sambamba na mkakati wa Tigo wa kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja na kutimiza ahadi yake ya kuwapatia wateja fursa ya kupata bidhaa na huduma kwa urahisi zaidi.

“Ahadi yetu kwa wateja ni kuwapa huduma za kibinafsi na kutoa suluhisho la duka moja kwa mahitaji yao yote. Kuongezeka kwa mahitaji ya huduma zetu kunatokana na hitaji la wateja kufuata mtindo wa maisha wa kidijitali.

“Duka hili jipya lina eneo maalum la matumizi ambapo wateja wanaweza kupata fursa ya kufanya majaribio na kupata uzoefu wa bidhaa mbalimbali za Tigo kama vile simu za mkononi.

Duka linapatikana kwa urahisi kwa wateja wanaotembelea duka la Palm village”, aliongeza Madati.

Naye kwa upande waje Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. FATMA NYANGASA aliipongeza Tigo kwa dhamira yao ya kuwekeza rasilimali zake ili kuhakikisha wateja wanapata huduma za kiwango cha Kimataifa.

“Huduma za wateja mara nyingi ndio kiini cha biashara ambacho hulenga kutoa huduma ya kipekee inayomwacha mteja anahisi kuthaminiwa na kuheshimiwa na Tigo ndiyo bora zaidi katika kuwekeza rasilimali zake katika kutengeneza uzoefu wa kukusudia mazuri kwa wateja,” Alisema Mwegelo.

Tigo ni mwanzilishi wa uvumbuzi nchini Tanzania. Duka hili ni la 54 nchini na ni uthibitisho mwingine kwamba Tigo ni kinara katika utoaji wa huduma za kidijitali kwa wateja wake.