January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tigo wazindua awamu ya pili mradi wa ‘Tigo Green for Kili, One Step One Tree’

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kampuni inayoongoza nchini Tanzania kwa utoaji wa huduma za kidijitali, Tigo Tanzania, leo imepanda miche ya miti 1,000 kama sehemu ya mradi wake unaoendelea wa Tigo Green for Kili, One Step One tree, katika mkoa wa Kilimanjaro. Upandaji wa miche 1,000 ya miti katika kijiji cha Kwa-Sadala wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro umeanza awamu ya pili ya mradi kwa mwaka 2022.

Mradi wa Tigo Green for Kili, One Step One Tree ulizinduliwa mwishoni mwa Februari 2021, kwa lengo kuu la kuhifadhi theluji na mimea kuzunguka Mlima Kilimanjaro. Katika awamu ya kwanza, Tigo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi na ya umma ilikusanya zaidi ya miche 30,000 ya miti lakini ilifanikiwa kupanda zaidi ya miche 11,000 ya miti.

Akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa upandaji wa miche hiyo katika eneo la Kwa-Sadala wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, Mkurugenzi wa Tigo Tanzania Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alisema, “Mradi wetu wa upandaji miti upo katika awamu ya pili. Tuliamua kuendelea na zoezi la upandaji miti katika msimu huu wa mvua ili miche istawi. Mwaka huu tunatarajia kupanda zaidi ya miche 20,000 ya miti ambayo itapunguza athari za ongezeko la joto duniani na kusaidia kurejesha theluji kwenye Mlima Kilimanjaro.”

“Napenda kuipongeza VOEWOFO kwa kuratibu na kuandaa jambo hili adhimu, kwa sababu imekuwa si jambo jepesi, ukizingatia hali ya hewa imekuwa si nzuri kwetu, kulikuwa na ukame katika maeneo mengi ya mkoa huu, lakini mwaka huu mambo yanaonekana kuwa mazuri. , ndiyo maana tunapiga hatua kwa kupanda miche 1,000 ya miti leo.”

Kutoka “Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) – Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini-Dkt. Lewis Nzali ambaye pia alikua mgeni rasmi katika tukio hili amesema kuwa ” mradi wa upandaji miti unaofadhiliwa na Tigo Tanzania. Mradi huu wa matarajio utahakikisha Kilimanjaro ya kijani kibichi kwa miaka ijayo”.

Lakini pia Meneja Rasilimali watu wa VOEWOFO, ambae pia ni mwanachama wa bodi ya VOEWOFO – Bi. Neema Mahimbo aliipongeza Tigo kwa kuendeleza mradi wake wa kuhifadhi mimea inayozunguka Mlima Kilimanjaro. “Tunatarajia kuendelea kufanya kazi na Tigo na wadau wengine, tunaporejesha mradi huu. Tunaamini kwamba kwa msaada wa Tigo, tuko karibu zaidi kufikia lengo letu na kuchangia Kilimanjaro yenye kijani kibichi kwa vizazi vijavyo”.