Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Kampuni inayoongoza nchini kwa utoaji wa huduma za Kidigitali Tigo , kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Samsung Tanzania wametambulisha rasmi simu janja tatu sokoni kwa mpigo , simu hizo ni SAMSUNG Galaxy A 33 , A53 pamoja na A73 ambazo kuanzia leo hii zinapatikana katika mabanda ya sabasaba pamoja na maduka ya Samsung na Tigo nchi nzima .
Akizungumza wakati wa kutambulisha simu hizo mpya sokoni Mkuu wa kitengo Cha Maduka na bidhaa za Intanet Tigo Tanzania Ndg Mkumbo Myonga amesema kuwa
” Simu hizi zina OFA maalumu ikiwa ni pamoja na punguzo BABKUBWA pamoja na vifurushi vya Intanet ambavyo ni GB 96 kwa mwaka mzima Bure kabisa”.
Kwa wateja wote watakaotembelea Banda la sabasaba wataweza kujipatia na zawadi ikiwa ni pamoja na saa ya feet 2 kwa wale watu wa mazoezi, vikombe, tisheti na zawadi nyingine kibao.
Tembelea maduka ya Tigo na mabanda ya sabasaba kwa simu Bomba na original zenye warranty ya miezi 24. ” Alimalizia .
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mauzo kutoka Samsung Bwn. Moses Mtweve ameongezea kuwa
” Simu hizi zina ubora wa kipekee zikiambatana na warranty ya miaka miwili pamoja na warrant ya kioo ambayo ni additional ya mwaka mzima ambapo mteja anapata zaidi ya 85% ambayo ni punguzo kwa simu hizi tatu.
Tunaendelea kuwasihi Watanzania waweze kuchangamkia fursa hii ya punguzo hasa katika msimu huu wa sabasaba ili waweze kujipatia simu hizi zenye ubora wa kipekee.
Alimalizia.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi