December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tigo na Infinix wazindua ” Infinix Smart 6 na Hot 12i “nchini Tanzania

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za kidijitali Tanzania, Tigo Tanzania, imeshirikiana na INFINIX Tanzania kuzindua INFINIX SMART 6 ambayo itauzwa kwa bei ya shilingi 220,000 na HOT 12i kwa Tsh 270,000.

Akizungumza katika uzinduzi huo , Mkuu wa Kitengo cha Maduka na Bidhaa za Intaneti kutoka Tigo,. Mkumbo Myonga amesema kuwa

“Tunafuraha tena kuungana na INFINIX Tanzania kuzindua simu mpya za kisasa ambazo zitaimarisha zaidi lengo letu la kuunganisha watanzania katika mfumo wa huduma za Kidigitali kote nchini. Na Mfumo huu unaimarisha zaidi imani ya washirika wetu hasa katika mtandao wetu wa 4G uliosambaa kote nchini”.

“Kulingana na mkakati wetu wa kuharakisha kupenya kwa simu za kisasa nchini huku tukihakikisha kuwa wateja wanafurahia matumizi bora ya kidijitali kupitia mtandao wa kasi zaidi wa 4G+ ambao ni mkubwa zaidi nchini, tunatoa GB 78 za intaneti BURE kwa muda wa mwaka mmoja kwa wateja wote watakaonunua simu janja za Infinix Smart 6 na HOT 12i.” alisisitiza Myonga.

Naye kwa Upande wake Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa, alisema kuwa

“Leo tumetangaza kuzindua simu mpya kabisa ya Infinix HOT 12i, simu mahiri mpya ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu kama zilivyo simu zetu siku zote, Infinix ina RAM ya kutosha, teknolojia ya fusion huruhusu simu za HOT 12i kuongeza RAM Mfano 3GB ya RAM inaweza kuongezwa mpaka kuwa 6GB ya Ram, Screen kubwa ya 6.6HD+” 90Hz Pro-Level ya elektroniki itakayokufanya ufurahie kucheza Game katika simu yako. Pia Inakuja na betri ya 5000mAh, Chipset Helio, itakayokufanya utumie simu yako katika masuala mbalimbali kama kucheza game , kuingia kwenye mitandao ya kijamii na mambo mengine mengi bila kuhofia chaji kuisha”,

“Tumejitolea daima kubuni simu mahiri zenye utendakazi bora na za kisasa kwa wateja wetu, huku zikiwa mpya zenye ubora wa hali ya juu na gharama nafuu kila wakati. Infinix HOT 12i na Smart 6 zimepata mafanikio katika utendakazi ulioboreshwa, ustahimilivu wa muda mrefu, muundo wa kisasa wa Smart 6 huku zikihakikisha ulinzi thabiti .

Tunawakaribisha wateja Wetu wote katika maduka ya Infinix na Tigo Nchini kujipatia simu hizi mpya na za kisasa na kufurahia maisha ya Kidigitali “.
Alimalizia Aisha Karupa.