December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TIGO kuzawadia wateja wake zaidi ya Milioni 325 katika “PESA MWAA MWII NA TIGO PESA”

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Dar es Salaam

KAMPUNI inayoongoza kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali Nchini Tigo Tanzania , kupitia mfumo wake wa huduma za kifedha wa Tigo Pesa leo wamezindua promosheni mpya ya wiki 5 inayojulikana kwa jina la “Pesa Mwaa Mwii na Tigo Pesa” ambayo itawawezesha wateja wa Tigo Pesa kuondoka na zawadi za fedha taslimu hadi Milioni 325/- .

Promosheni hiyo, ambayo inatokana na mafanikio ya ofa ya Tigo Pesa ya kutimiza miaka 10 iliyozinduliwa mwaka jana ili kuwahimiza wateja kutumia suluhu za malipo ya kidijitali katika miamala yao ya kila siku. Wateja wa Tigo Pesa wanastahili kuingia kwenye droo na kujishindia zawadi za fedha taslimu kwa kufanya miamala tofauti tofauti kama vile Lipa Kwa Simu, Malipo ya Bili, Malipo ya Serikali, miamala ya mtandaoni , na kupokea pesa kutoka kwa mtandao mwingine wa simu.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Promosheni hii Afisa Mkuu wa Tigo Pesa Bi. Angelica Pesha amesema kuwa

“Tigo Pesa kwa miaka mingi imechangia katika ajenda ya kitaifa ya ujumuishi wa kifedha na kupitia bidhaa na huduma zetu za kibunifu zinazomlenga mteja tumefikisha huduma dhabiti za kifedha kwa zaidi ya wateja milioni 9. Tumeona ukuaji wa utegemezi wa huduma za kifedha kwa simu za mkononi nchini kote na promosheni ya Pesa Mwaa Mwii na Tigo Pesa inajikita katika dhamira yetu ya kukuza malipo ya kidijitali nchini kote kwa kutumia suluhu mbalimbali za kidijitali zinazowezesha watumiaji katika ulimwengu unaozidi kuwa wa kidijitali”, alisema, Bi . Angelica Pesha.

“Promosheni hii ya Pesa Mwaa Mwii na Tigo Pesa ni maalum kwa wateja wa Tigo Pesa, ambapo tutakuwa na jumla ya washindi 111, washindi 20 wakishinda 2M kila wiki kwa wiki 5, washindi 10 kupata zawadi kubwa ya 10M mwisho wa promosheni. na mshindi 1 wa jumla akipata 25M. Wateja wanahimizwa kufanya miamala mingi iwezekanavyo kutoka kwa huduma zilizotajwa hapo juu ili kupata nafasi ya kuwa mamilionea. Alieleza Pesha.
“Tigo Pesa imebadilisha maisha ya mamilioni ya wateja nchini Tanzania na kutokana na kuongezeka kwa ujuzi wa kidijitali na kupenya kwa simu za mkononi, suala linaloifanya Tigo Pesa kuwa watoa huduma za kifedha kikamilifu wanaounganisha wateja katika ulimwengu wa kifedha wa kidijitali,” Pesha alibainisha.

Mteja anachotakiwa ni kufanya miamala mara nyingi iwezekanavyo kupitia huduma za Tigo Pesa (Lipa Kwa Simu, Malipo ya Bili , Malipo ya Serikali, Mtandao wa rika kwa rika, kupokea kutoka mitandao mingine ya simu) zilizopo ili kupata nafasi ya kushinda. zawadi za fedha.

Afisa Mkuu wa Tigo Pesa,Angelica Pesa akitambulisha promosheni mpya iitwayo Pesa Mwaa Mwii na Tigo pesa,pembeni ni Meneja wa wateja maalumu wa TigoPesa Mary Rutta