March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tido ateuliwa kuwa mshauri wa RaiS,habari na mawasiliano

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan,amemteua Tido Mhando kuwa Mshauri wa Rais, Habari na Mawasiliano.

Taarifa iliotolewa leo Novemba 19,2025 na ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Dkt.Moses M. Kusiluka,imesema mbali na Tido,pia Rais Dkt.Samia amemteua 

 Bakari  Machumu, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu. 

Machumu anachukua nafasi  Sharifa Bakari Nyanga ambaye amepangiwa majukumu mengine.

Pia amemteua  Lazaro Samuel Nyalandu  kuwa Balozi.