Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Taasisi ya The Angeline Foundation imetoa msaada wa sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kwa watoto yatima wanaolelewa katika vituo mbalimbali wilayani Ilemela, Mkoa wa Mwanza, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha watoto hao wanasherehekea sikukuu katika mazingira salama.

Msaada huo umetolewa Desemba 24,2025 na Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dkt. Angeline Mabula kupitia Mratibu wa The Angeline Foundation,Charles David,ambao umejumuisha chakula cha sikukuu pamoja na mahitaji ya shule ikiwemo madaftari kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, ili kuunganisha furaha ya sikukuu na maandalizi ya mwendelezo wa masomo.
akizungumza kwa njia ya simu,Dkt.Angeline,amewahimiza watoto hao kusoma kwa bidii ili kila mmoja atimize malengo yake huku akiwaasa kulinda amani Iliyopo kwa kuishi kwa kufuata malezi na upendo wanaopewa na walezi wao.
Awali akizungumza wakati wa ugawaji msaada huo Mratibu wa The Angeline Foundation,Charles David,amesema, taasisi hiyo imekuwa na utaratibu wa kila mwaka kushiriki chakula pamoja na watoto wanaotoka katika mazingira magumu na vituo vya kulelea watoto.
Pamoja na kuendesha bonanza la Krismasi jambo ambalo liliwafanya watoto kushiriki pamoja na jamii na kupata burudani pamoja.
Pia amesema kwa mwaka huu taasisi hiyo imeamua kuja na utaratibu wa kuhakikisha watoto hao wanafikiwa katika vituo vyao ambapo wamepatiwa mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula watakachotumia katika kusherekea sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya pamoja na mahitaji ya shule ikiwemo madaftari kwa wananfuzi wa msingi na sekondari.

Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Phonelisco,ameishukuru taaisisi hiyo kwa kuwa na utaratibu wa kuwafulia mara kwa mara na kuwapatia mahitaji ya msingi na kukisikia faraja.
Mbali na mahitaji hayo pia taasisi hiyo ilikuwa imeisha kabidhi magodoro ,nishati mbadala(gesi) pamoja na viti kwa ajili ya kuendelea kutoa msaada katika vituo hivyo vya kulelea watoto.


More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi