January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

THBUB yalisifu jeshi la Polisi kwa utendaji kazi wake

Na Mwandishi wetu Timesmajira Online

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nchini(THBUB) imesema Jeshi la Polisi Nchini limekuwa linafanya kazi zake vizuri licha ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kutokana na uwepo chagamoto za maadili kutoka kwa baadhi ya askari wake.

Kutokana na hatua hiyo imelitaka Jeshi la Polisi nchini kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za jeshi ili kuepuka vitendo vya uvunjifu wa haki za Binadamu.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu,Mathew Mwaimu wakati akitoa taarifa ya Tathmini kuhusu mwenendo na utendakazi wa Jeshi ilo nchini kuanzia mwaka 2020 hadi 2022.

Jaji Mwaimu amesema Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora ilifanya uchunguzi 10 zinazihusu tuhuna dhudi ya hilo pamoja na kutembelea vituo vya polisi katika baadhi ya mikoa nchini.

Amesema katika uchuguzi THBUB iliweza kubaini kupigwa na kuteswa kwa watuhumiwa wakati Ukamataji au wakati wa upelelezi ukiendelea ,kuwepo tuhuma za Rushwa dhidi ya baadhi ya askari.

“Tathimini ya ujumla wake imesema kwa mazingira ya utendaji wa jeshi la Polisi wanatekeleza kazi zao vizuri licha ya kuwepo kwa baadhi chagamoto ambazo ujitokeza za kimaadili kwa baadhi ya askari wake mmoja mmoja au kikundi na kusababisha kulipaka Jeshi matope”amesema Jaji Mwaimu

Pia amesema chugunzi nyingine ni Pamoja na baadhi ya askari Polisi kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu vitendo wanavyolalamikiwa na wananchi, askari Polisi wanaopatikana na hatia kupewa adhabu isiyowiana na kosa husika .

Jaji Mwaimu aliendelea kueleza kuwa baadhi ya watuhumiwa kuwekwa mahabusu za polisi kwa muda mrefu bila ya kupelekwa mahakamani au kupewa dhamana.

Aliongeza kuwa uhaba vitendea kazi, uchache wa nyumba za kuishi askari, uchache wa Askari Polisi na miundombinu chakavu katika vituo vya Polisi.

Akitaja mikoa ilikofanyika chugunzi hizo ni katika wilaya Kinondoni, Ubungo, na ilala katika mkoa wa Dar es salaam na kwa Mkoani ni Wilaya ya Mwanga katika mkoa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Kilosa na Mvomero katika mkoa wa Morogoro.

Pia Mikoa mingine ambayo THBUB ilifanya uchuguzi ni Wilaya ya Tabora Mjini kwa Mkoa wa Tabora Wilaya ya Mafinga kwa Mkoa wa Iringa, Wilaya ya Handeni Kwa mkoa wa Tanga , Wilaya ya Masasi kwa Mkoa wa Mtwara na Mkoa wa mjini Magharibi Zanzibar.

Aidha,Jaji Mwaimu amelitaka jeshi la polisi kuzingatia sheria ya Jeshi la polisi na huduma saidizi sura ya 322,sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai sura 20 na kanuni za jeshi la polisi za mwaka 2013 ambazo zimeainisha kazi za jeshi .

Katika hatua nyingine aliiomba serikali kuimarisha Jeshi la Polisi kwa kulipatia vitendea kazi kuendelea kuwajengea makazi bora, kuongeza idadi ya Askari Polisi na kuimarisha miundombinu.

Mwenyekiti Tume ya haki za binadamu na utawala Bora (THBUB) Jaji mstaafu Mathew Mwaimu (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa tathimini kuhusu mwenendo na utendaji kazi wa jeshi la Polisi Nchini