Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) imezindua Vitabu vya Nukta nundu, Flashi na Redio zenye ujumbe wa Lishe kwaajili ya watu wa jamii ya wasioona nchini lengo likiwa ni kuhakikisha Watanzania wote wanakabiliana na tatizo la Utapiamlo na Udumavu.
Uzinduzi huo umefanywa na Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani SARAH GIBSON ambao wameshiriki kufanikisha mpango huo ambapo amepongeza Tanzania kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia watu wasiona kupata taarifa sahihi za Lishe kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa.
Akizungumza katika uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo na Elimu ya Lishe wa taasisi hiyo Esther Nkuba amesema matarajio yao ni kwamba jamii ya watu wasioona watanufaika na elimu pamoja na taarifa sahihi za lishe na hivyo kuchochea mabadiliko ya tabia kuhusu kufuata taratibu sahihi za lishe ikiwemo ya mjamzito na maama anayenyonyesha.
“Watu hawa wapo milioni 2.9, hili ni jambo muhimu sana ili kuwafikia watu hawa, kitabu hiki tulichozindua kinahamaisha na kuwaelimisha watu wasioona kuhusu umuhimu wa Lishe bora kwa ustawi, ukuaji na maendeleo ya watoto na afya ya jamii hiyo kwa ujumla”
“Kwa muda mrefu jamii ya watu wasioona imekua ikikabiliana na changamoto ya upatikanaji wa taarifa za lishe kwasababu taarifa nyingi za lishe zimeandikwa kwa maandishi ambayo hawawezi kuyasoma wala kuyaona, ambapo hupata taarifa kupitia vyombo vya habari hususani Runinga, Radio na mitandao ya kijamii ambapo kwa asilimia kubwa hukosa kupata taarifa za lishe kwa usahihi”
Pia Nkeba alisema ni matarajio yao kwamba jamii ya watu wasioona watanufaika na elimu hiyo pamoja na taarifa za lishe ambazo zitawasaidia kujenga uelewa kuhusu umuhimu wa lishe kwa afya zao na hivyo kuchochea mabadiliko ya tabia kuhusu kufata mtindo bora wa maisha.
Nkuba alisema Tasisi imeendelea kufikia makundi mbalimbali kwenye jamii ikiwemo wanawake wajawazito na wanyonyeshao lakini pia wanawake wenye umri wa kuzaa, watoto wachanga, vijana balehe na wazee.
Aliwashukuru wadau wote wa Lishe wakiwemo wadau wa Afya, watumishi wa Taaisisi ya Chakula na Lishe Tanzania, wizara mbalimbali za kisekta, idara na taasisi za umma, asasi zq kiraia na wadau wa maendelo kwa mchago wao mzima katika kuinua hali ya lishe nchini hasa kwa kuendelea kutoa huduma na kufanikisha huduma za lishe nchini.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu Wasioona Tanzania OMARY ITAMBU ameishukuru taasisi ya Lishe na Chakula kuona umuhimu wa kuwafikia watu wasioona huku akiziomba taasisi nyingine kuhakikisha jamii hiyo pia inafikiwa katika masuala mbalimbali na hivyo kwenda pamoja.
Kwa Upande wake mwakilishi mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani Bi. Sarah Gordon-Gibson amesema waliamua kuunganisha nguvu na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania ili kuweza kuandaliwa kwa nyezo hizo zenye ujumbe wa lishe kwa watu wasioona, mara baada ya kugundua jamii hiyo inakosa fursa ya kupata elimu sahihi kuhusu masuala ya chakula na lishe.
“Watu wenye matatizo ya kuona hawawezi kupata taarifa za lishe kupitia vyombo vya habari vya magazeti, kama vile mabango, vipeperushi na vipeperushi. Kwa hivyo, ilikuwa ni lazima kuendeleza afua zinazofaa na zilizolengwa ili kuwahimiza kufuata tabia na mitindo ya maisha chanya ya lishe.” Alisema Bi.Gordon.
Zaidi ya watu laki mbili nchini wanakabiliwa na tatizo la kutoona na hivyo kukosa taarifa sahihi za masuala ya Lishe hususan vijijini.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato