December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi wa Ufundi TFF,Oscar Milambo

TFF yatoa ufafanuzi CV za makocha

Na Mwandishi Wetu, Times Majira Online

SHIRIKISHO la Soka nchini Tanzania TFF, limetolea ufafanuzi juu ya agizo la klabu zote kuwasilisha wasifu wa makocha wake kwa mkurugenzi wa Ufundi wa TFF.

TFF ilitoa agizo hilo jana kuwa Vilabu viwasilishe vyeti na wasifu wa makocha wao kwa mkurugenzi wa ufundi,Oscar Milambo na mwisho wa kuwakilisha wsifu Septemba 15 mwaka huu.

Hata hivyo Mirambo afafanua mara baada ya kuulizwa kwa nini agizo hilo limetolewa wakati ligi imeshaanza alisema inawezekana tamko hilo lakini ni suala la msingi ni kutaka kuhakikisha makocha wanakidhi vigezo vilivyowekwa.

Milambo amesisitiza kwamba vipo vilabu ambavyo bado havijawasilisha wasifu ingawa ni utaratibu ambao upo kila msimu.