Mario Balotelli
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester City na Liverpool Mario Balotelli amefanya mazungumzo na timu ya Championi ya Barnsley. Muitalia huyo mwenye umri wa miaka 30 , yuko huru baada ya mkataba wake na Bresica kusitishwa kwa kutohudhuria mazoezi . (Sun)
Klabu ya Chelsea wanataka kusaini mkataba na kiungo wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, mwenye umri wa miaka 17 badala ya kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 21. (Eurosport)
Kocha wa Man City Pep Guardiola, bado hajaamua kuhusu hali yake ya baadaye katika klabu hiyo. Ambapo mkataba wake unaisha msimu huu. (Goal)
Leicester wanamfuatilia kwa karibu kiungo wa safu ya ulinzi Nuno Mendes, mwenye umri wa miaka 18 raia wa Ureno, ambaye anakipengele cha kumnunua cha pauni milioni 40 katika mkataba wake na Sporting Lisbon. (Mail)
Kiungo wa kati wa zamani wa Juventus Claudio Marchiso amemtaka mchezaji wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 27, arejee katika klabu hiyo ya Italia . (Mirror)
Klabu ya Man United watapata kipaumbele mauzo ya wachezaji mwezi wa Januari huku mlinzi wa England Phil Jones, mwenye umri wa miaka 28, na Muagerntina mlinda lango Sergio Romero, 33, na beki Marcos Rojo,30, wakiwa na uwezekano mkubwa wa kuondoka katika klabu hiyo. (Manchester Evening News)
Mazungumzo ya mkataba wa Watford na winga Adama Traore yamekwama kwasababu Muhispania huyo hafurahii muda anaopewa kucheza gemu . Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 awali alihusishwa na taarifa za kuhamia Barcelona. (Goal)
West Ham wamepewa ofa ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Real Mdrid Muhispania Mariano Diaz, 27.
Arsenal wanaangalia uwezekano wa kufanya mkataba wa kubadilishana wachezaji na Inter Milan ambao utamuwezesha Mdenmark na mlinzi wa zamani wa Tottenham Christian Eriksen, 28, kujiunga na the Gunners na kiungo wa kati Mswiss Granit Xhaka, 28, kuhamia katika klabu hiyo ya Italia . (Corriere dello Sport, via Talksport)
Arsenal wako katika mazungumzo ya kumuuza beki Mfaransa William Saliba kwa mkopo msimu ujao. (Evening Standard)
Meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte anasema alitaka kusaini mkataba na mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk na Romelu Lukaku wa Inter Milan wakati alipokuwa katika klabu hiyo . (Telegraph)
Mshambuliaji wa Chelsea raia wa Ufaransa Olivier Giroud, 34, atakwenda mapumzikoni mwezi Januari kama muda wake wa kucheza hautaongezwa katika kipindi cha miezi ijayo . (The Athletic – subscription retired)
Arsenal hawatamsaini Mitchel Bergkamp – mtoto wa kiume wa mchezaji wa zamani wa Gunners Dennis Bergkamp – licha ya kwamba Muholanzi huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akifanyiwa majaribio ya kimchezo kwa wiki moja katika klabu hiyo.
%%%%%%%%%%%%%
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania