January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Eduardo Camavinga

Tetesi za soka Ulaya leo Jumanne 13.10.2020

Eduardo Camavinga

MANCHESTER United ipo kwenye mipango ya kumsainisha kiungo wa Rennes raia wa Ufaransa Eduardo Camavinga, mwenye umri wa miaka 17, iwapo kiungo wa timu hiyo Paul Pogba, ataamua kuondoka Old Trafford. (Sport Witness)

Hata hivyo Manchester United huenda ikakabilana na Real Madrid katika kumuwania Camavinga. (Star).

Uhamisho wa mshambuliaji wa Algeria Said Benrahma wa pauni milioni 25 kutoka Brentford kwenda West Ham uko hatarini kuvunjika, kwani mpango wao umeelekeza zaidi kwa mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Josh King, mwenye umri wa miaka 28. Crystal Palace huenda ikapeleka ofa ya lala salama kumnasa Benrahma, 25. (Mirror)

Manchester City itajaribu tena kumsajili mlinzi wa kushoto wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico, mwenye umri wa miaka 28, mwezi January. (Sun)

Milan Skriniar

Klabu ya Tottenham huenda ikarejesha nia yake ya kumsajili mlinzi wa kati wa Inter Milan raia wa Slovakia Milan Skriniar, mwenye umri wa miaka 25, mwezi January. (Team Talk)

Nayo klabu ya Fulham wako katika hatua nzuri ya mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Huddersfield raia wa Uholanzi Terence Kongolo, mwenye umri wa miaka 26. (Football Insider)

Wachezaji kadhaa wa Manchester United wameeleza masikitiko yao ya namna hali inavyomwendea mlinda mlango wa timu hiyo muargentina Sergio Romero, mwenye umri wa miaka 33, ambaye amekosa nafasi Old Trafford baada ya kurejea kwa Dean Henderson, lakini uhamisho wake wa siku ya mwisho kushindikana kufuatia ada iliyowekwa ya pauni milioni 10. (ESPN)

Baba wa kiungo wa Arsenal raia wa Ghana Thomas Partey amesema, mtoto wake alikuwa anasubiri timu kubwa imfuate licha ya Juventus na Chelsea kuonyesha nia ya kumtaka. (Mirror)

Naye kiungo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani anayechezea Arsenal Mesut Ozil, 31, ambaye hajacheza kikosi cha kwanza tangu mwezi Machi, mwishoni mwa Septemba alilipwa marupurupu ya mrahaba yanayofikia pauni milioni 8. (The Athletic – subscription required)

Beki wa Aston Villa raia wa Ufaransa Frederic Guilbert, mwenye umri wa miaka 25, ameapa kupambania nafasi yake ndani ya klabu hiyo, baada ya uhamisho wake kuelekea Nantes kukwama kwenye dirisha la usajili la majira ya joto. (Express and Star)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City raia wa Brazil Robinho, mwenye umri wa miaka 36, amejitolea kupokea mshahara wa pauni 200 tu kwa mwezi akirejea kwa awamu ya nne kwenye klabu yake ya utotoni Santos. (Manchester Evening News)

Mtendaji mkuu wa Portsmouth Mark Catlin amesisitiza kwamba kutakuwa na wachezaji wapya Fratton Park kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Ijumaa. (The News)