Jadon Sancho
Klabu ya Manchester United wiki ijayo itaweka mezani dau la mwisho la puani milioni 90, kwa ajili ya kumsajili winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 20 raia wa England. (Mirror)
Arsenal wameonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Chelsea raia wa Italia Jorginho, mwenye umri wa miaka 28. (Sky Sports – via Mail)
Lucas Torreira
Kiungo wa Asernal Lucas Torreira anakaribia kuondoka katika klabu hiyo huku klabu za Atletico Madrid na Torino zikionyesha nia ya kumnasa kiungo huyo wa Uruguay, mwenye umri wa miaka 24. (Independent)
Hata hivyo klabu ya Atletico Madrid wanaamini watamnasa Torreira kwa mkopo, hatua itakayoifanya Arsenal nayo kumsajili kiungo wa timu hiyo Thomas Partey, mwenye umri wa miaka 27, raia wa Ghana. (Sky Sports)
Alex Telles
Mlinzi wa kushoto katika klabu ya FC Porto, inayoshiriki Ligi Kuu Ureno Alex Telles, mwenye umri wa miaka 27 raia wa Brazil, anaamini kiwango cha fedha kilichotajwa na klabu yake kwa Manchester United cha pauni milioni 18.3, sio halisi kwa sababu atakuwa mchezaji huru msimu ujao. (Guardian)
Klabu ya Manchester City imesema, madai kwamba imeweka ofa ya pauni milioni 78, kwa ajili ya mlinzi wa Atletico Madrid raia wa Uruguay Jose Gimenez, mwenye umri wa miaka 25, sio kweli. (Goal)
Dele Alli
Monaco imeonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Tottenham raia wa England Dele Alli, mwenye umri wa miaka 24, (90min)
Hata hivyo Paris St-Germain wanatarajia kujiondoa kwenye mazungumzo ya kumsajili Alli kwa mkopo wa muda mrefu. (Telegraph – subscription required)
Mshambuliaji wa Chelsea raia wa England Callum Hudson-Odoi, mwenye umri wa miaka 19, anataka kuondoka Stamford Bridge kwa mkopo . (Talksport)
Philippe Coutinho
Naye kiungo mchezeshaji wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 28, anaweza kwenda kwa mkopo Arsenal kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Star)
Klabu ya RB Leipzig, wanakaribia kumsajili mlinzi wa kati, hatua itakayosaidia mlinzi wake Dayot Upamecano kuondoka klabuni hapo huku Manchester United imekuwa ikihusishwa kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21. (Star)
Carlo Ancelotti
Mshambuliaji wa Napoli Arkadiusz Milik amewekwa sokoni kwa kikosi cha Everton cha Meneja Carlo Ancelotti, lakini Muitaliano huyo akiwa na joto la kutaka kuungana nae tena nyota huyo wa kimataifa wa Poland, mwenye umri wa miaka 26. (Corriere della Sera – via Inside Futbol)
Klabu ya Sheffield United inaongoza mbio za kumsajili mshambuliaji wa Liverpool raia wa Uingereza Rhian Brewster, mwenye umri wa miaka 20, huku klabu za Aston Villa, Brighton na Crystal Palace zikionyesha nia ya kumsajili. (Independent)
West Ham na Aston Villa ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka kumsajili kiungo wa Chelsea raia wa England Ruben Loftus-Cheek, 24, kwa mkopo wa msimu mzima. (Guardian)
Southampton ni miongoni mwa vilabu vinavyomuania Loftus-Cheek . (Mail)
Ibrahim Sangare,
Hata hivyo klabu hiyo ya Southampton wanatarajia pia kukamilisha usajili wa kiungo wa Toulouse raia wa Ivory Coast Ibrahim Sangare, mwenye umri wa miaka 22. (Telegraph – subscription required)
Nayo klabu ya Everton na Fulham wanamuania mlinzi wa Cameroon Jerome Onguene mwenye umri wa miaka, 23, kutoka RB Salzburg. (Sportslens)
Emmanuel Adebayor
Klabu ya West Brom wanaweza kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester City Emmanuel Adebayor, mwenye umri wa miaka 36, kama watashindwa kumnasa mshambuliaji mwingine kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Sun)
Mlinzi wa St Etienne Wesley Fofana anaweza kutua Leicester City lakini mpango wowote utakaokubaliwa utakaomfanya kinda huyo wa umri wa miaka 19 asalie kwenye Klabu hiyo ya Ufaransa. (L’Equipe – via Leicester Mercury)
Meneja wa Southampton Ralph Hasenhuttl anataka kusajili wachezaji watatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Daily Echo)
Klabu ya Bayern Munich hawatamruhusu kiungo wa Ufaransa Michael Cuisance kuondoka kwa mkopo, licha ya Leeds United na Marseille kuripotiwa kuonyesha nia ya kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 21. (Sport Bild – in German)
%%%%%%%%%%%
More Stories
Naibu Waziri wa Fedha abariki ujio mpya wa Bahati Nasibu
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes