Milan Skriniar
Klabu ya Inter Milan wapo mbioni kumuuza mlinzi wa klabu hiyo raia wa Slovakia Milan Skriniar, mwenye umri wa miaka 25, kwenda Tottenham kwa pauni milioni 45 mwezi ujao. (Sun)
Mlinzi wa kati wa Uholanzi Perr Schuurs, mwenye umri wa miaka 21, aliyehusishwa na taarifa za kuhamia Liverpool, anasisitiza kuwa hayuko tayari kuondoka Ajax. (Mirror)
Meneja wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino yuko mbele ya kocha wa kikosi cha akiba cha Real Madrid Raul kama mgombea anayeongoza miongoni mwa wagombea wanaowania kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane, iwapo Real wataamua kumfuta kazi Mfaransa huyo. (Marca)
Hata hivyo, Pochettino anahusishwa kutaka kuhamia Paris St-Germain na anaweza kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel. (Talksport)
Klabu ya West Ham wako katika mazungumzo na meneja David Moyes kuhusu kuongezwa kwa mkataba wake , ambao unamalizika msimu huu . (Sky Sports)
Zidane
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amepoteza imani na wachezaji wake kadhaa ikiwa ni pamoja na winga wa zamani wa Chelsea Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 29, ambaye pia mchezaji wa kimataifa kutoka Ubelgiji. (Sport)
Zidane anaungwa mkono na bodi ya Real Madrid na wachezaji kwa sasa, lakini hali yake katika timu hiyo ya siku zijazo inaweza kuamliwa na mechi tatu zijazo za timu hiyo. (ESPN)
Kocha msaidizi wa Aston Villa John Terry anamtafuta mchezaji mwenza wa zamani katika timu ya Chelsea Ashley Cole kushikilia nafasi ya kazi katika utawala wake wa timu kama atateuliwa kuchukua kazi ya kudumu ya kocha Phillip Cocu. (Mirror)
Meneja wa Tottenham Jose Mourinho anasema ni jukumu lake kuamua iwapo klabu hiyo itamuuza kiungo wa kati wa England Dele Alli, mwenye umri wa miaka 24, mwezi Januari au la (Telegraph – subscription required)
Newcastle wamekuwa wakimfuatilia kwa karibu mchezaji wa Manchester United Brandon Williams huku kijana huyo mwenye umri wa miaka 20- anayecheza safu ya ulinzi wa kushoto katika kikosi cha vijana waliochini ya umri wa miaka 21 cha England anaweza kupatikana kwa mkataba wa mkopo mwezi wa Januari. . (Newcastle Chronicle)
Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anasema yeye pamoja na mkururugenzi wa masuala ya kiufundi Edu wanafanya mpango kwa ajili ya kipindi cha dirisha la uhamisho mwezi Januari na kile kinachoweza kuwa soko ”lisilotarajiwa” (London Evening Standard)
Werder Bremen wameachana na mpango wa kumuuza kiungo wa kati Mkosovo Milot Rashica mwezi Januari licha ya taarifa kwamba Aston Villa wanaweza kurejea nia yao kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 . (Birmingham Mail)
Leicester City wanaweza tena kuwa na haja na mchezaji wa kati Mreno William Carvalho, mwenye umri wa miaka 28, huku Real Betis wakipanga kumuuza Januari. (La Razon, via Leicester Mercury)
Kiungo wa kati na mshambuliaji wa Timu ya Ufaransa Houssem Aoaur, 22, ambaye alihusishwa na timu ya Arsenal katika msimu huu, anasema anafurahia kwamba aliendelea kubakia katika klabu ya Lyon. (RMC Sport, via Get French Football News)
Primia Ligi haitajaribu kutoa chanjo za Covid-19 kwa wachezaji wa soka kabla ya kutolewa kwa chanjo hizo kwa watu wote . (Telegraph)
Watangazaji wamejipanga kuendelea kutoa kelele bandia kwa ajili ya soka katika televisheni, licha ya kurejea kwa mashabiki.
Televisheni za Sky Sports na BT Sport zitatumia mchanganyiko wa kelele kutoka kwa mashabiki, ambazo zimekuwepo katika mechi tangu mechi ziliporejea viwanjani bila mashabiki mwezi Juni . (London Evening Standard)
%%%%%%%%%%%%%%%%%
More Stories
Naibu Waziri wa Fedha abariki ujio mpya wa Bahati Nasibu
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes