December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sadio Mane

Tetesi za soka Ulaya leo Alhamisi 24.09.2020

Alex Telles

Mlinzi wa FC Porto inayoshiriki Ligi Kuu Ureno mwenye umri wa miaka 27 raia wa Brazil, Alex Telles, inadaiwa anataka kuondoka klabu hiyo na kujiunga na Manchester United, ambao wanajaribu kushawishi uongozi wa Porto ili kupunguziwa dau lake la pauni milioni 36 (Telegraph ).

Sadio Mane

Klabu ya Liverpool wanatazamiwa kumtumia mshambuliaji Sadio Mane kumshawishi mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Senegali Kalidou Koulibaly ili atue klabuni hapo kutoka Napoli, licha ya Manchester City na Paris St-Germain kuonyesha nia ya kumsaini mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 29. (Le Parisien, via Sun)

PSG wanamtaka beki wa Chelsea Mjerumani Antonio Rudiger, mwenye umri wa miaka 27, kwa mkopo wa msimu mzima. (Mail)

Chris Smalling

Klabu ya FC Roma inayoshiriki Ligi Kuu Italia Serie A, wapo mbioni kuweka ofa ya pili kwa ajili ya mlinzi wa Manchester United na timu ya Taifa ya England Chris Smalling, mwenye umri wa miaka30, ambaye aliichezea timu hiyo ya ligi ya Serie A kwa mkopo msimu uliopita. (Guardian)

Lucas Torreira

Nayo Atletico Madrid wanalenga kumsajili kiungo wa Arsenal na timu ya Taifa ya Uruguay Lucas Torreira, mwenye umri wa miaka 23. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Klabu ya West Ham wako tayari kupambana na Manchester United kwa ajili ya kupata saini ya beki wa kati wa Swansea City raia wa Wales Joe Rodon, mwenye umri wa miaka 22. (Guardian)

West Ham United, pia imeweka ofa yenye thamani ya pauni milioni 33, kwa ajili ya mlinzi wa kati wa Saint-Etienne Wesley Fofana, mwenye umri wa miaka 19, ambaye anawaniwa pia na Leicester City. (Sky Sports)

Klabu ya Burnley, nao wako kwenye mazungumzo na Liverpool kuhusu kumsajili winga wao Harry Wilson, mwenye umri wa miaka 23 raia wa Wales. (Independent)

Lazio imefikia makubaliano na Southampton kwa ajili ya kunasa saini ya mlinzi wao Wesley Hoedt, mwenye umri wa miaka 26, raia wa Uholanzi, kurejea kwenye klabu hiyo ya Italia kwa mkopo. (Sky Sport Italia – in Italian)

Klabu ya Barcelona na Bayern Munich zimeweka ofa ya kumsajili Mlinzi wa kulia wa Ajax raia wa Marekani Sergino Dest, mwenye umri wa miaka 19. (Marca)

Mario Gotze

Bayern Munich, imewasiliana na Mario Gotze kuhusu kujiunga tena na klabu hiyo. Mshambuliaji huyo raia wa Ujerumani, mwenye umri wa miaka 28, ni mchezaji huru baada ya kuondoka Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu uliopita. (Sport Bild – in German)

Mlinzi wa kulia wa Atletico Madrid raia wa Colombia Santiago Arias, mwenye umri wa miaka 28, amewasili Ujerumani kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na Bayer Leverkusen. (Marca)

Mshambuliaji wa zamani wa Italia Francesco Totti anatarajiwa kurudi Roma kama mkurugenzi wao mkuu wa michezo. (Corriere dello Sport – in Italian).

%%%%%%%%%%%%%%%