January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tetesi za soka Ulaya

Philippe Coutinho

Mchakato wa winga wa Barcelona Philippe Coutinho kuhamia Arsenal unaelekea kukamilika. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil msimu uliopita alikuwa Bayern Munich kwa mkopo. (Sport)

Arsenal imetoa ofa ya miaka mitatu kwa winga wa Chelsea na Brazil Willian, 31. (Sky Sports)

Chelsea iko katika mazungumzo ya hatua ya mwisho na beki wa kushoto wa Real Madrid Sergio Reguilon, 23, ambaye msimu uliopita alikuwa Sevilla kwa mkopo. (ESPN)

Marc-Andre Ter Stegen and Manuel Neuer

Manuel Neuer (kushoto) na Marc-Andre ter Stegen (kulia)

Mlinda lango wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen yuko tayari kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu ya Uhispania. Hatua hiyo itakatisha tamaa Chelsea, ambayo ilikuwa inamfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 28, (Mundo Deportivo via Sun)

Tottenham inamnyatia winga wa Brentford na Algeria Said Benrahma, 24. (Mirror)

Jason Tindall, 42, ndio anayepigiwa upatu kwa kiasi kikubwa kuchua nafasi ya Eddie Howe kama kocha wa Bournemouth. (Telegraph)

Scott Parker

Fulham itampa ofa kocha Scott Parker ya mkataba mpya baada kushinda kwenye mashindano ya michuano. (Express)

Werder Bremen inataka kumchukua winga wa Manchester United, 20, Tahith Chong kwa mkopo. (Bild – in German)

Aston Villa itashindana na Crystal Palace kumng’ang’ania mshambuliaji wa Brentford, Ollie Watkins, 24, ambaye anaweza kuondoka the Bees kwa pauni milioni 18 baada ya kushindwa kufuzu kupandishwa daraja kwenye Ligi ya Premier. (Express and Star)

Ryan Fraser
Maelezo ya picha,Ryan Fraser alikuwa amepata goli moja tu kwa timu ya Bournemouth

Crystal Palace imetoa mkataba kwa winga wa Scotland Ryan Fraser, 26, ambaye sasa yuko huru baada ya kuondoka Bournemouth. (Guardian)

Fulham itajaribu kuingilia hatua ya Southampton ya kutoa ofa ya pauni milioni 12 kwa beki wa Tottenham Kyle Walker-Peters, 23, aliyekuwa kwa mkopo St Mary msimu uliopita. (Evening Standard)

Mchezaji wa Real Madrid James Rodriguez, 29, amepangiwa kuhamia kwa mahasimu Atletico Madrid kwa kitita cha pauni milioni 13.5. (El Golazo de Gol via Sun)

Serge Aurier
Maelezo ya picha,Serge Aurier beki wa kulia wa Tottenham na pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast

Tottenham iko tayari kumuuza beki wa kulia anayesemekana kwamba thamani yake ni pauni milioni 35 Serge Aurier, 27, huku AC Milan na Monaco zote zikionesha nia ya kumpata raia huyo wa Ivory Coast. (Mirror)

Na Tottenham iko tayari kumuuza beki wa kati wa Marekani Cameron Carter-Vickers, 22 kwa kitita cha karibu pauni milioni 2.5. (Football Insider)