January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tetesi za soka Ulaya

José Mourinho anataka kumrejesha Tottenham mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 31. (Cuatro-in Spanish). Beki wa kati wa Paris St -Germain Thiago Silva, 35, ambaye anaondoka kwenye klabu hiyo ya Ufaransa baada ya fainali za michuano ya klabu bingwa Ulaya amepewa ofa na Chelsea (Telegraph).

Gareth Bale

Kushindwa kufikiwa kwa maelewano binafsi ya mkataba wa Muingereza Jadon Sancho, 20 kumeongeza ugumu wa uhamisho wake kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester United (ESPN).

Jadon Sancho
Maelezo ya picha,Mshambuliaji wa Borrusia Dortmund jadon Sancho

Manchester United wanaweza kuipatia Aston Villa mlinda mlango Sergio Romero,33, kama sehemu ya makubaliano ili kumpata kiungo wa kati Jack Grealish, 24. (Mail). Chelsea na Atletico Madrid wana mpango wa kumpata winga Federico Bernardeschi, 26, anayekipiga Juventus. ( Calciomercato-in Italian).

Liverpool inajiandaa kumuuza kiungo Marko Grujic, 24, na winga Harry Wilson, 23, msimu huu (Mirror).

Kai Havertz scores from the penalty spot
Maelezo ya picha,Havertz alipata goli baada ya kupata penalti, mbele ya wachezaji wa Borussia Monchengladbach

Chelsea watakamilisha kumsajili kiungo wa kati wa Kijerumani Kai Havertz, 21, wiki hii kwa mkataba wa miaka mitano iwapo wao na Bayer Leverkusen wanaweza kupunguza tofauti ya pauni milioni 18 ya thamani ya mchezaji huyo. (Telegraph).

Kiungo wa kati wa Manchester United Mbrazili Andreas Pereira, 24, analengwa na Benfica na Valencia. (ESPN). United imerejesha shauku yao kwa beki wa kushoto Alex Sandro, 29, anayeichezea Juventus ( Calciomercato-in Italian).

Ben White
Maelezo ya picha,Leeds imetoa ofa ya tatu kwa Ben White huku Newport, Peterborough pia zikiwa zimeonesha ya kumsajili

Leeds imetoa ofa ya tatu-inayoaminika kuwa takribani pauni milioni 25 kwa ajili ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi Ben White, 22. (Sky Sports).

Tottenham inataka kumchukua mshambuliaji wa Liverpool Rhian Brewster, 21 kwa mkopo. (Football Insider).

Wolves wako tayari kusikiliza ofa kubwa kwa ajili ya winga Adama Traore ingawa mchezaji huyo, 24, bado amesalia na miaka mitatu ya kuutumikia mkataba wake. (Mail).

Adama Traore
Maelezo ya picha,Adama Traore amekuwa sehemu kubwa ya mazungumzo ya Wolves

West Ham inataka kumuuza mshambuliaji Jordan Hugill, 28, msimu huu. Hugill aliutumia msimu uliopita akichezea QPR kwa mkopo. (Evening Standard).

Fulham imeuliza mustakabali wa mlinzi wa kati wa Barcelona Gerard Pique, 33 (Libero-in Spanish). Fulham na Wolves huenda wakachuana na Everton kupata saini ya Kiungo wa kati wa Watford Abdoulaye Doucoure, 27. ( Evening Standard).

Bournemouth wanajiandaa kutoa ofa kwa ajili ya mlindamlango wa Wigan David Marshall, 35. (Football Insider).

Ryan Kent (left) celebrates his goal
Maelezo ya picha,Ryan Kent (kushoto) akisherehekea baada ya kufunga goli

Cottagers wameingia pia katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth Muigereza Callum Wilson, 28. (Telegraph).

Leeds inatayarisha kitita cha pauni milioni 10 kwa ajili ya winga wa Rangers, Ryan Kent, 23. (Sun).

Kocha wa zamani wa England Sven Goran Eriksson anajiandaa kuwa kocha mpya wa Jamaica. ( Mirror).

Chelsea itafanya mazungumzo na kiungo wa kati Conor Gallagher huku Newcastle na Crystal Palace zote zikionesha nia ya kumsajili msimu uliopita .

Mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala

Burnley inafanya mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Angers, Baptiste Santamaria. Raia huyo wa Ufaransa, 25, alikuwa gumzo kwasababu ya kitita cha pauni milioni 12 na Aston Villa mwaka jana. (RMC Sport, via Daily Mail)

Brighton inasema nahodha Lewis Dunk, 28, na mlinzi Ben White, 22, watasalia katika klabu hiyo. Dunk amehusishwa na Chelsea huku Leeds ikiwa inataka kufanya mazungumzo na White. (Talksport)

Everton na Napoli pia nazo zinamnyatia Mbrazili Gabriel Magalhaes

Arsenal ina matumaini ya kukamilisha makubaliano ya pauni milioni 22 kwa mlinzi wa Lille Gabriel Magalhaes. Everton na Napoli pia nazo zinamnyatia mchezaji huyo wa Brazil, 22. (ESPN)

Na, Juventus huenda ikamtumia mshambuliaji Paulo Dybala, 26, kama sehemu ya makubaliano ya mabadilishano na Manchester United kumrejesha Paul Pogba katika Ligi ya Serie A. Raia wa Argentina Dybala amesalia na miaka miwili huko.