Arsenal ina matumaini ya kukamilisha makubaliano ya pauni milioni 22 kwa mlinzi wa Lille Gabriel Magalhaes. Everton na Napoli pia nazo zinamnyatia mchezaji huyo wa Brazil, 22. (ESPN)
Chelsea itakamilisha makubaliano ya mchezaji wa Bayer Leverkusen Kai Havertz, 21, ndani ya siku 10 zijazo. Raia huyo wa Ujerumani anataka kuhakikishiwa makubaliano ya miaka mitano huko Stamford Bridge. (Bild, via Express)
Juventus huenda ikamtumia mshambuliaji Paulo Dybala, 26, kama sehemu ya makubaliano ya mabadilishano na Manchester United kumrejesha Paul Pogba katika Ligi ya Serie A. Raia wa Argentina Dybala amesalia na miaka miwili huko.
Wakati huohuo, Man Utd inamfuatilia winga wa Brazil na Juventus, 29, Douglas Costa. (Sky Sports)
Watford imekataa kitita cha kwanza kutoka Everton kwa ajili ya kiungo wa kati Abdoulaye Doucoure. Hornets inataka kima cha pauni milioni 25 kwa mchezaji huyo, 27, wa Ufaransa. (Standard)
Lazio inafikiria kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na Brazil Felipe Anderson, 27, baada ya David Silva kuwachezea shere dakika za mwisho. (Star)
Chelsea itafanya mazungumzo na kiungo wa kati Conor Gallagher huku Newcastle na Crystal Palace zote zikionesha nia ya kumsajili msimu uliopita .
Burnley inafanya mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Angers, Baptiste Santamaria. Raia huyo wa Ufaransa, 25, alikuwa gumzo kwasababu ya kitita cha pauni milioni 12 na Aston Villa mwaka jana. (RMC Sport, via Daily Mail)
Brighton inasema nahodha Lewis Dunk, 28, na mlinzi Ben White, 22, watasalia katika klabu hiyo. Dunk amehusishwa na Chelsea huku Leeds ikiwa inataka kufanya mazungumzo na White. (Talksport)
Aston Villa ina imani kubwa ya kuendelea kuwa na kiungo wa kati Douglas Luiz, 22. Raia huyo wa Brazil alikuwa amehusishwa na kurejea Manchester City. (Express and Star)
Sheffield United inafikiria kutoa ofa ya mkopo kwa mlinda mlango wa Manchester United Dean Henderson, 23, licha ya kukubaliana kwa kitita cha pesa cha uhamisho na Bournemouth kwa ajili ya Aaron Ramsdale, 22. (ESPN)
Norwich inamlenga West Ham mshambuliaji Jordan Hugill, 28. (Mail)
Southampton inafanya mazungumzo na Schalke juu ya makuabliano ya pauni milioni 20 kwa kiungo wa kati wa Marekani Weston McKennie, 21. (Sky Sports)
Fulham na Crystal Palace ambazo zimepandishwa daraja tu hivi karibuni zina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Peterborough raia wa Ivory Coast Siriki Dembele, 23. (Football Insider)
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania